Katibu Mtendaji Idara ya Habari na Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Anatoly Salawa, akifungua mkutano wa umoja wa wanamawasiliano katoliki Tanzania. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mawasiliano Katoliki Tanzania (UMAKATA), Gaudence Hyera. Mkutano huo unafanyika Tabata jijini Dar es Salaam zilipo ofisi za Tumaini Media.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Jimbo Katoliki la Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Tumaini Media, Padri Paul Haule akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mtendaji Idara ya Habari na Mawasiliano, Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Anatoly Salawa, kufungua mkutano huo. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mawasiliano Katoliki Tanzania (UMAKATA), Gaudence Hyera.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao ni wajumbe wa UMAKATA wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambao ni wajumbe wa UMAKATA wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa sakafu katika mkutano huo, Modesti Msangi (kulia) akitoa taarifa fupi ya UMAKATA kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Meza kuu kabla ya kuanza kwa mkutano huo.