Ulemavu wa Kuzaliwa Tatizo Kubwa kwa Watoto Duniani

Ulemavu wa Kuzaliwa Tatizo Kubwa kwa Watoto Duniani
WATOTO huchukuliwa kama taifa la kesho duniani kote hivyo basi kuwapatia huduma ya afya sahihi lazima ipewe kipaumbele . Mahitaji ya afya ya watoto ni ya kipekee sana, na ya tofauti sana ukilinganisha na watu wazima kwahiyo yanahitaji bidii sana. Mara kwa mara kumekuwepo matukio kadhaa ya kuzaliwa kabla wa wakati, uzito mdogo wa kuzaliwa, mtoto kuzaliwa na kisukari, pumu, uzito na unene uliopitiliza, watoto walioungana na kasoro nyingine nyingi.

Kasoro hizi za kuzaliwa zinaripotiwa mara kwa mara kutishia maisha ya watoto wachanga na hivyo basi kuhitaji matibabu ya haraka. Kasoro hizo zinaenda zikitofautiana kutoka kasoro ndogo ambazo hazina haja ya matibabu makubwa na kubwa ambayo zinaweza kusababisha ulemavu. Mapungufu haya yanakuwepo tangu kuzaliwa kwa mototo na kwa kawaida husababishwa na mapungufu katika jeni, matatizo ya kromosomu, urithi, Teratojeni au upungufu wa virutubisho(i) Kuna aina mbili kuu za ulemavu wa kuzaliwa; kimuundo na kazi /maendeleo.
Watoto walioathirika na ulemavu wa kimuundo kawaida huwa na tatizo katika sehemu yao ya mwili yaani kiungo au mfumo. Kasoro hizi ni pamoja na viungo visivyokuwa vya kawaida na kasoro katika moyo. Ulemavu wa kuzaliwa aina ya pili unaohusiana na kazi au maendeleo mara nyingi hudhihirishwa na matatizo katika uendeshaji wa sehemu ya mwili au mfumo katika mwili. Ulemavu huu ni pamoja na matatizo katika mfumo wa neva, ubongo, hisia (kuona, kusikia nk), metaboli na matatizo upunguvu (ii)
Ulemavu wa kuzaliwa ni moja ya vitu vinavosababisha vifo kwa watoto wachanga duniani. Madhara yake hujidhihirisha zaidi kwa nchi zinazoendelea ambapo miundombinu yake ya huduma ya afya haijakuwa.Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathirika na tatizo hili, kumekuwepo na matukio mengi nay a kuhudhunisha yatokanayo na tatizo hili. Mwanzoni mwa mwez January mwaka huu walizaliwa watoto mapacha walioungana hospital ya Mara na baadae kuhamishiwa katika hospital ya bugando. Hata hivyo hospitali hizo hazikuweza keshughulikia afya zao.

Taarifa ya Shirika la afya duniani(WHO) limeonyesha kuwa Tanzania imekuwa na maendeleo mazuri katika kupunguza vifo kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka vifo 112 kwa kila watoto 1000 kama ilivyoripotiwa mwaka 2005 na kufikia vifo 81 kwa kila watoto 1000 mwaka 2010. Vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja imepungua pia kutoka 68 na kufikia 51 kwa kila watoto 1000 kwa muda huohuo.(iii)

Hivi karibuni, kumekuwapo na kampeni ya chanjo kitaifa iliyofanyika ili kuwalinda watoto milioni 21 dhidi ya surua na rubella magonjwa ambayo ni michango mikubwa wa ulemavu kwa watoto wachanga. Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO), Gavi, shirika la chanjo na washirika wengine walifanya kampeni Oktoba 2014 ilikiwa ni sehemu ya Malengo ya millenia (MDG’s ) ya kupunguza vifo vya watoto nchini (iv).
Hosipital kubwa duniani yenye maono ya kugusa maisha ya watoto wadogo na wanaoishi katika mazingira magumu, hosipitali ya watoto ya Apollo ni mfano wa kuigwa kwa jinsi ilivyoweka kipaumbele katika kutoa huduma za watoto. Hosipitali hiyo iliyopo nchini India inatoa huduma ya afya madhubuti kwa watoto wote kuanzia mwaka 0 mpaka 16. Huduma hizo hujumuisha vipimo mara kwa mara ili kugundua tatizo mapema, huduma za kinga na chanjo, ushauri wa lishe, elimu ya afya, mafunzo kitabia na utafiti. Tanzania na nchi nyinginezo duniani zina nafasi ya kuiga njinsi ya kutoa huduma za afya kwa watoto kutoka kwa hospitali hiyo inayoongoza kwa huduma za afya iliyosheheni madaktari na wataalamu bingwa
Uhusiano uliopo kati ya hospitali hiyo na nchi ya Tanzania ni mkubwa na wagonjwa mbalimbali hupatiwa rufaa kwa ajili ya kuhuduma za matibabu ya juu zaidi. Pamoja na mafanikio makubwa yaliyodhihirishwa na hospitari hiyo katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni katika kuhudumia watoto wagonjwa kutoka Tanzania, juhudi zake katika kuboresha huduma za afya ya mtoto haziwezi kupuuzwa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kutenganisha mapacha kutoka Tanzania wajulikanao kwa jina la kitaalamu Pygopagus, Ericana na Eluidi Desemba mwaka 2013. Mafanikio hayo yalidhihirishwa tena mwaka 2014 kwa kutenganisha mapacha wajulikanao kitaalamu kama thoraco-omphalopagus, upasuaji uliochukua zaidi ya masaa 11 na jopo la madaktari bingwa wa hospitali hiyo.
Hosipitali ya watoto ya Apollo ipo katikati ya mji wa Chennai, nchini India, Umbali wa kutupa jiwe kutoka hospitali ya Apollo, Hospitali hiyo ya watoto ina vitanda 80, na madaktari bingwa waliobobea katika kutoa huduma za afya kwa watoto (v). Idara ya watoto ina wataalamu mbalimbali kamadara vile wataalamu wa magonjwa ya moyo, magonjwa ya watoto wachanga, upandikizaji, afya ya akili na pia hutoa huduma za kuanzia huduma za kinga, tathmini za ustawi, matibabu ya magonjwa sugu na madogo, yanayotishia maisha kwa makundi yote ya umri wa mtoto. Kutoka kijusi, watoto waliozaliwa, watoto wachanga, watoto chin ya miaka mitano, kabla ya kuanza shule, umri wa kwenda shule kwa vijana kila mmoja kulingana na mahitaji yao ya afya ya kipekee.
Ulemavu wa kuzaliwa unakadiriwa kutokea kwa mtoto 1 katika kila watoto wachanga 33 wanaozaliwa. Takriban watoto milioni 3.2 huzaliwa na ulemavu kila mwaka. Zaidi ya watoto 270,000 hufa katika siku 28 za kwanza kila mwaka kutokana na kasoro za kuzaliwa. Mapungufu hayo yanaweza kusababisha ulemavu wa muda mrefu ambao unaweza kuwa na madhara makubwa kwa watu binafsi, familia, mifumo ya huduma za afya na jamii. Ingawa kasoro hiyo inaweza kuwa ya kurithi au zitokanazo na mazingira katika asili mara nyingi ni vigumu kubainisha sababuau chanzo halisi (vi).
Madhara yatokanayo na ulemavu wa kuzaliwa ni makubwa sana katika nchi zakipato cha kati na chini ambapo asilimia 94% ya watoto wa aina hii hutokea huku. Takriban 95% ya watoto ambao wanakufa kutokana na ulemavu wa kuzaliwa ni kutoka nchi hizi. Maambukizi halisi ya tatizo hili katika Afrika inaweza kuwa tofauti na nchi zilizoendelea, kutokana na tofauti katika jeni na vichochezi kama vile maambukizi. Mwaka 2013, matokeo ya utafiti uliofanywa katika hospitali ya Bugando nchini Tanzania na Dr.Florentina Mashuda ilionyesha kuwa mzunguko wa kasoro ya kuzaliwa uilikuwa 128 kati ya watoto 445 sawa na asilimia (28.8%) ya watoto wachanga waliolazwa hospitali ya Bugando. (vii).
Mwaka huu kutakuwa na majadiliano muhimu juu ya ulemavu wa kuzaliwa kufuatia kuwepo kwa semina ya kwanza kanda Afrika juu ya ulemavu wa kuzaliwa itakayofanyika mjini Arusha, Tanzania Machi 2015. Mkitano huo utashirikisha Shirika la kimataifa la ufuatiliaji na utafiti wa Madhara ya Uzazi, Shirika la Afya Duniani, Shirikisho la Kimataifa la spina bifida na ubongo, na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC). Malengo ya warsha hiyo ni kuleta ufahamu juu ya maswala ya kasoro za kuzaliwa Africa, kusaidia nchi zilizoshiriki kuendeleza mipango yao ya sasa juu ya kasoro kuzaliwa ufuatiliaji na kusaidia kushughulikia haja muhimu kwa ajili ya kuondoa kabisa tatizo hili. Warsha ya pili imepangwa kufanyika wakati mwingine katika Septemba mwaka 2015 Dar-es-Salaam (viii).
Kwa msaada wa vifaa vya kisasa na teknolojia hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto, matatizo ya maumbile na ulemavu wa kuzaliwa inaweza kugundulika tangu motto akiwa tumboni. Watu wakitaka kuwa wazazi, ni muhimu kwao kujua baadhi ya hatua zichukuliwe kupunguza, kuzuia na kugundua kasoro za kuzaliwa katika hatua za mwanzo za ujauzito.
Lakini pia ni muhimu kutambua kwamba watoto wengi wenye kasoro za kuzaliwa wanazaliwa na wazazi wawili wenye afya wasiokuwa na matatizo ya afya dhahiri au dalili hatarishi. Aidha, vipimo mara kwa mara kwa akina mama wajawazito ni muhimu kwa ajili ya kuelewa maendeleo ya mtoto tumboni.