Ukosefu wa Elimu ya Biashara Wawakwaza Wanawake EAC

Nembo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Na Baltazar Nduwayezu, EANA

UFAHAMU wa mfumo wa biashara na sheria za forodha ni mahitaji muhimu kwa wafanyabiashara wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kama wanataka kunufaika na biashara katika kanda hiyo.

Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) Andrew Luzze alipokuwa anahutubia warsha ya siku tatu ya Jukwaa la Wafanyabishara Wanawake wa Afrika Mashariki (EAWiBP) mjini Arusha iliyohudhuriwa na wajumbe 100 kutoka nchi wananchama wa EAC.

Kutoka na utafiti wa kanda ulifanywa kuhusu vikwazo vya biashara zinazomilikiwa na wanawake imebainika kuwa moja ya udhaifu ni kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya ufanyaji biashara katika kanda na pia kutojua sheria na sera husika za biashara.

Ili kukabiliana na vikwazo hivyo, Luzze alisisitiza umuhimu wa “kuongeza uelewa wa masuala ya biashara, hususan katika sheria za forodha za EAC na uongozi wa biashara.”

Warsha hiyo ililenga kuzichambua changamoto hizo kutoka na ukweli kwamba wafanyabishara wanawake kutoweza kuwa huru kusafirisha biashara zao ndani ya nchi tano wanachama wa EAC kutokana na kukosa elimu ya biashara. Nchi wanachama za EAC ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi.

Licha ya sera nzuri za biashara zilizomo kwenye mkataba wa EAC juu ya nafasi ya wanawake, takwimu zinaonyesa kwamba ushiriki wa wafanyabishara wanawake katika biashra ndani ya ka nda unajikita zaidi kwenye biashara zizizorasmi maeneo ya mipakani na ujasilimiamali mkubwa, mdogo na wa kati.

“Biashara zinazomilikiwa na wanawake zinaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo: sera duni za jinsia, upatikanaji hafisu wa masoko kitaifa, kikanda na kimataifa, tofauti kubwa za kijinsia, kutokuwa na uhakika wa umiliki wa ardhi na mali, upatikanaji hafifu wa huduma za mikopo na kutokuwa na elimu na ujuzi wa biashara,” ulifafanua utafiti huo.

Warsha hiyo ilidhaminiwa na EABC, Trade Mark East Africa, the African Capacity Building Foundation na African Women Development Fund.