PROMOTA wa muziki jijini Koloni Bw. Peter Betram (Mjerumani), amejikuta akiwekewa
masharti magumu katika juhudi zake za kutaka kuandaa onesho kubwa la muziki
katikati ya Jiji la Koloni, nchini Ujerumani. Kwa muda wa miaka miwili sasa poromota huyo amekuwa akiilalamikia Halmashauri ya Jiji la Koloni kwa kumwekea ngumu katika kuandaa onesho la muziki kwa visingizio anuai.
Kuanzia mwaka 2012 aliambiwa apeleke orodha ya bendi anazohitaji kuzipandisha jukwaani, baada ya kuonekana jina la Bendi ya Ngoma Africa katika orodha hiyo, Serikali ya jiji hilo ilimwagiza mtayarishaji wa onyesho hilo akubali kuingia gharama za ziada kwa ajili ya kuweka ulinzi kutoka na msongamano wa washabiki.
Hata hivyo alipewa sharti lingine kuwa onesho hilo liwe nje ya Mji na sio kitovuni mwa jiji, kutokana na kuepuka msongamano wa washabiki wa Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni yenye uwezo wa kuvuta mashabiki wake. Poromota amejikuta akivimba macho na kutojua nini cha kufanya.
Wadaku walipomtafuta kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja kutaka kupata mtazamo wake, alijibu kuwa kikosi chake kipo tayari na wakati wowote ule watakapoitwa na poromota huyo, Ras akunja watafanya kazi. Pamoja na hayo alikiri kuwa muda wa miaka miwili Poromota amekuwa akiwapigia simu, na bendi ipo tayari kama matayarisho yatakamilika alisema Kamanda Ras Makunja.
Mdodosa habari alipo hoji suala la kulikoni kamanda kumiliki bundi katika himaya ya “Anunnaki Empire” Kamanda Ras Makunja alikata simu..!!! sijui kama aliishiwa chaji au aliondoka ki – FFU kwa mwendo wa kasi!? Any way tuwatafute kambini kwao www.ngoma-africa.com
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa ngoma za kitamaduni mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola (CHOGM)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiongea na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Defue mara baada ya kuwasili jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 14, 2013 tayari kwa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola (CHOGM