UKATILI DHIDI YA BINADAMU!

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (International court of criminal- ICC, the Hagu, Netherlands) bwana Luis Moreno-Ocampo, amesema kiongozi wa Libya Gaddafi pamoja na viongozi kadhaa waandamizi, watachunguzwa kwa kosa la mashambulizi ya watu waliokuwa wakiandamana kwa njia ya amani. Swali langu hapa ni je hii mahakama ilishindwa nini kumchunguza rais Kikwete wa Tanzania ambaye serikali yake ilihusika moja kwa moja na mauaji ya watu waliokuwa wakiandamana kwa njia ya amani pale Arusha. Je hii mahakama haikuwa na habari na yaliyojiri?au pengine mahakama hii inafanya kazi kwa maslahi yake binafsi na upendeleo? Sipati jibu hapa!