Ukaguzi Maalumu Akaunti ya Tegeta Escrow

Nembo ya Bunge la Tanzania

Nembo ya Bunge la Tanzania

Hadidu Rejea
 
1)  Kuchunguza uendeshaji wa mkataba wa kuzalisha Umeme kati ya kampuni ya IPTL na TANESCO
 
2)  Kuchunguza kama wakati escrow inafunguliwa kampuni ya mechmar ilikuwa inamiliki IPTL, kama ilikuwa imefilisiwa na kama ilikuwa imehamisha umiliki wake kwa kampuni ya PAP.
 
3)  Kuchunguza na kuthibitisha ushahidi wa kampuni ya PAP kununua kampuni ya mechmar na kumiliki IPTL
 
4)  Kuchunguza chanzo cha mgogoro kuhusu tozo kati ya TANESCO na IPTL na kuthibitisha ushahidi wowote kuwa mgogoro uliamuliwa kwa faida ya IPTL
 
5)  Kuchunguza kama ilikuwa sahihi kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kusamehe kodi ya VAT ya jumla ya tshs 26 bilioni kutokana na tozo ya capacity charges na TRA wachukue hatua gani kuhakikisha kodi hiyo inakusanywa
 
6)  Kuchunguza kiwango cha fedha kilichopaswa kuwemo katika akaunti ya escrow, kiwango gani kilikuwepo wakati IPTL wanalipwa na kiwango gani kitapaswa kulipwa zaidi kutoka tanesco
 
7)  Kuchunguza madai ya benki ya standard chartered kwa tanesco na madai mengine yeyote yanayohusiana na mkataba wa kuzalisha Umeme wa IPTL na iwapo Serikali imejihadhari na uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa, nafasi na heshima ya nchi katika kuheshimu mikataba ya kimataifa na ya uwekezaji.
 
8)  Kuchunguza iwapo Wizara ya Nishati na madini ambayo ni mhusika Mkuu wa akaunti ya tegeta escrow ilifanya ‘due diligence’ ya kutosha kabla ya kuingia makubaliano ya kutoa fedha zilizopo akaunti ya tegeta escrow. Kupata Maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na madini ni kwa nini aliagiza ukaguzi maalum wakati yeye ni mhusika Mkuu kwenye mchakato mzima na ilhali akijua PAC tayari imeanza mchakato wa ukaguzi.
 
9)  Kutoa mapendekezo ya njia bora za kisheria kulinda Taifa kutoingia hasara zaidi katika mkataba wa IPTL chini ya wamiliki wapya
 
10) Kutoa ushauri kwa kamati ya PAC juu ya mapendekezo ya hatua ambazo Bunge linapaswa kuchukua kuhusu matokeo ya ukaguzi huu maalumu
 
Imetolewa na; KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)