Ujumbea wa Katibu Mkuu wa UN, Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

SIKU ya Redio Duniani inatambua nafasi ya kipekee na athari za chombo ambacho kinawafikia wasikilizaji wengi zaidi duniani kote.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaweka umuhimu katika haja ya watangazaji wa redio kila mahali kukuza sauti za wanawake na kuongeza nafasi wa wanawake ndani ya mashirika ya utangazaji.

Masafa ya redio mara nyingi yamekuwa nyuma linapokuja suala la usawa wa kijinsia.
Sauti za wanawake hazisikiki vya kutosha – ama mbele au nyuma ya kipaza sauti.
Hakuna habari za kutosha zinazoelezwa kuhusu wasichana na wanawake.

Wanawake ni robo tu ya wajumbe wa bodi kwenye kampuni za biashara za vyombo vya habari duniani. Navihamasisha vituo vya redio kuwa na umoja zaidi kwa kuwatambua kwa usawa wanawake miongoni mwa wafanyakazi wao na wasikilizaji wao.

Redio pia inaweza kusaidia kuondoa utengenezaji wa programu za kibaguzi na zisizo na usawa.
Hii ni fursa kwa kila mtu. Tuadhimishe siku hii ya Redio Duniani kwa kuonesha heshima kwa wanawake redioni – na kufanya makubwa kukuza sauti mpya za kesho.

Ban Ki-moon, Katibu Mkuu, Umoja wa Mataifa.

The 2014 theme is, “Gender Equality and Women’s Empowerment in Radio”. More information on WRD is available at: http://www.unesco.org/new/en/world-radio-day

Key Message
Radio owners, executives, journalists and government are urged to:
– Develop gender-related policies and strategies for radio
– Eliminate stereotypes and promote multidimensional portrayal in radio
– Build radio skills with a focus on young women as producers, hosts, and reporters
– Promote safety of women radio journalists