Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Liberata Mulamula pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico, Liberata Mulamula akimsikiliza kwa makini Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, Paul Mwafongo.
Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa, Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Silvacius Likwelile, Mkurugenzi wa Idara ya kupunguza Umasikini MKUKUTA Bi. Anna Mwasha pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya wakisikiliza kwa makini.
Ujumbe wa Tanzania wakisikiliza kwa makini hoja zinazotolewa na Waziri wa Fedha hayupo pichani ambaye ni mwenyekiti wa kikao hicho.
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo wakisikiliza kwa makini.