KESHO ni siku ya Siku Kuu, pasi na shaka hakuna mtu ambaye halijui hilo. Siku Kuu ya Chrismas na mwaka mpya ni siku kuu ambazo hufuatana na kwa desturi ya ushirikiano tulio nao hapa nchini siku hizi hatubagui hatuchagui kila mtu hufurahi pamoja na mwenzake.
Furaha hii ni pale wana jamii walio na mirengo tofauti ya kiimani wanapojumuika pamoja na kufurahia, waumini wa dini ya Kikristo walio wengi kesho wanasherehekea kuzaliwa kwa Masia Yesu Kristo.
Lakini kidoogo tujikumbushe kuzaliwa kwa Yesu Kiristo kulikuaje; Maandiko matakatifu kutoka katika Kitabu cha Biblia Matayo 1:18-21 kunaelezea wazi namna Yesu Kristo alivyo zaliwa.