Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Juma Changa akionyesha jinsi wazee wa zamani walivyokuwa wakichonga mpini wa jembe kwa kutuma teso “menzo” wakati mpiga picha wetu alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila la wasafwa huku Said Mbata (kulia), Victoria Zitta Mnyanyi (katikatia) na Sosteli Mponzi (kushoto) wakimuangalia. Ujenzi wa kituo hicho unajengwa kwa kujitolea na Mponzi ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kulia) akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi (kushoto) ambaye ni Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya moja ya nyumba ya kale iliyokuwa inatumiwa na kabila la wasafwa ambalo ni kabila maarufu mkoani humo. Mponzi ameamua kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ambacho kitatunza kumbukumbu za utamaduni na mila zote ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakimuangalia Mary John akisaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe aina ya “Lwala” wakati walipotembelea ili kujionea ujenzi wa kituo cha utamaduni wa kabila lao kinachojengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi. Baadhi ya wasafwa waishio maeneo ya vijijini bado wanasaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe hilo kwa ajili ya kutengenezea pombe. Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo