Ujenzi Mabondeni Waendelea Pamoja na Maafa ya Mvua Zilizopita!

20140526-160900.jpg

20140526-160917.jpg

20140526-160926.jpg

20140526-160936.jpg

Pamoja na notisi iliyobandikwa tarehe 13.5.2013, ikiwataka wabomoe majengo hayo. Wakazi hao wamepuuza notisi hiyo, na sasa nyumba hizo zimekamilika na wakazi wameshahamia.

Mwandishi alishuhudia nguo zikiwa zimeanikwa na ndoo zikiwa zimewekwa nje kwa ajili ya matumizi ya Kila siku. Hili ni eneo la Kigogo, pembezoni mwa mapito ya Mto Msimbazi. Eneo hilo wakati wa mvua ni ukanda wa Maji kuelekea baharini.

Mamlaka husika zisifumbie macho jambo hili. Tahadhari kabla ya hatari, na kinga ni bora kuliko tiba.

Picha na Habari na Mdau Maalum wa Thehabari, Dar.