Uhakiki wa Mipaka Mgogoro wa Ardhi Kinyenze

Ofisa Ardhi Wilaya ya Mvomero, Majaliwa Jafari (mwemnye miwani kulia) akitoa maelezo juu ya ramani ya shamba 296 lililopo Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero mkoani Morogoro ambalo lina mgogoro baada ya Mwekezaji wa Kizungu wa kudaiwa kuvamia mashamba ya wananchi na kufunga njia inayounganisha kitongoji cha Kinyebnze na mwanga kijijini Kipera. Kulia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha mwanga na katikati yao ni Mwanakijiji Mroki Mroki.

OFISA Mtendaji wa Kata ya Mlali, Said Said Mdume akizungumza na maofisa ardhi na wananchi wa Kinyenze baada ya zoezi la upimaji kusitishwa kufuatia wananchi kutaka zoezi hilo lifuate mchoro uliopo unaonesha mpaka wa shamba hilo ni barabara ya waenda kwa miguu na lipo mbali na Mto Kinyenze na sio kama ilivyo pimwa na kuvuka mto.

Akina mama na watoto wakifuatilia zoezio hilo

Maofisa wa Ardhi Wilaya ya Mvomero wakiwa katika uhakiki wa mipaka hiyo kijijini hapo jana.