Ufaransa Yaweka Ulinzi Mkali Michuano ya Euro

euro

Ufaransa inakabiliwa na changamoto yake kuu ya kwanza ya usalama wakati wa dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2016. Tamasha la wazi la ufunguzi linaandaliwa Paris katika eneo lenye uwezo wa kuwa na watu 90,000

Baada ya maandalizi ya muda mrefu ambayo yamekabiliwa na changamoto chungu nzima, hatimaye dimba la EURO 2016 linaanza kutifua vumbi Ijumaa nchini Ufaransa. Lakini katika habari ambayo huenda isiwafurahishe mashabiki ni kuwa wamiliki wa mabaa na mikahawa hawatoruhusiwa kuziweka nje skrini za televisheni wakati wa kipindi kizima cha michuano hii.

Hatua hiyo tata inalenga kuimarisha usalama wakati wa dimba hilo la mwezi mzima, wakati maafisa wa Ufaransa wanataraji kuwa watu wachache watakusanyika nje ya maeneo rasmi ya kukutana mashabiki ikiwa skrini za televisheni za nje zitapigwa marufuku.

Maeneo ya mashabiki kawaida huwekwa katika kumbi za wazi au bustani karibu na miji mikuu ya mji, na kuwawezesha mashabiki kutizama mechi kwenye skrini kubwa za televisheni. Hatua za zoada za usalama, ikiwemo mifumo ya video za siri, zimeongezwa ili kuweka usalama katika maeneo ya mashabiki.

Leo usiku, Dj maarufu wa Kifaransa David Guetta atautumbuiza umati chini ya mnara wa Eiffel mjini Paris, siku moja kabla ya wenyeji Ufaransa kushuka dimbani dhidi ya Romania katika mpambano wa ufunguzi wa kinyang’anyiro hicho uwanjani Stade de France.

Serikali ya Ufaransa imezindua app ya smartphone isiyo na malipo katika lugha ya Kifaransa na Kiingereza ambayo itawaonya wageni dhidi ya “mgogoro wowote mkuu”, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kutokea mashambulizi.

Wenyeji wa michuano hii Ufaransa watafungua pazia kwa kushuka dimbani kuwakabili Romania katika mechi ya kundi A mchezo ukichezwa katika dimba la Stade de France Mjini Paris.

Jumla ya 24 zitashiriki michuano hii na ikiwa ni mara ya kuweza kushirikisha idadi ya timu hizo hapo awali ni timu 16 tu ndizo zilikua zinacheza michuano hii.

Viwanja kumi vikitumika kumsaka bingwa mpya wa ulaya,mabingwa watetezi wa mashindano haya ni Spain ambao walibeba Kombe Mwaka 2012.