Ufaransa imeanza vizuri mashindano haya ya kombe la mataifa ya Ulaya jana Ijumaa , kwa timu yake ya taifa kuishinda Romani kwa mabao 2-1 na majeshi ya usalama yakisimama imara na kuhakikisha kwamba kila mtu anakuwa salama katika viwanja na mitaani ambako mashabiki walisheheni katika maeneo mbali mbali wakiangalia mtanange huo.
Miezi saba baada ya uwanja wa mpira kulengwa katika mashambulizi ambayo yalisababisha watu 130 kuuwawa mjini Paris, taifa hilo wenyeji wa Euro 2016 lilifungua mashindano hayo yanayoshirikisha timu 24 kwa bao la dakika za mwisho na kuishinda Romania kwa mabao 2-1
Mchezaji huyo wa kati wa Ufaransa alimimina krosi ambayo Olivier Giroud aliiweka wavuni kwa kichwa katika dakika ya 58 na kufunga bao la kwanza katika fainali hizi za mwaka huu na kisha Payet binafsi alipachika bao la ushindi baada ya Bogdan Stancu kusawazisha kwa Romania kwa mkwaju wa penalti.