Uchaguzi Mkuu; ZEC Yatakiwa Kushirikiana na NEC

Ufunguzi wa mkutano wa 'forum' ya viongozi wa Tume za Uchaguzi za Jumuia ya Afrika Mashariki

Ufunguzi wa mkutano wa ‘forum’ ya viongozi wa Tume za Uchaguzi za Jumuia ya Afrika Mashariki

TUME za Uchaguzi katika Jumuia ya Africa Mashariki zimetakiwa kushirikiana na kutoa ushirikiano kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanziba (ZEC) katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Africa Mashariki Bwana Charles Njoroge wakati wa ufunguzi wa mkutano wa forum ya viongozi wa Tume za Uchaguzi za Jumuia hiyo uliofanyika katika hoteli ya New Africa Hoteli jijini Dar es Salaam leo.

“Uenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ni nafasi nyeti na ina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kijamii na kisiasa , ni matumaini yangu kwamba iwapo tutaungana na kufanya kazi pamoja jumuia ya Africa Mashariki Forum na kushirikiana kuweka nguvu katika kuendesha chaguzi kutakuwa na ufanisi , uhuru na haki katika chaguzi zetu na kufikia malengo tunayoyataka” Alisema Njoroge.

Uchaguzi nchini Tanzania mwaka huu umekuwa na hamasa kubwa ukilinganisha na chaguzi zilizopita katika nyanja mbalimbali ikiwepo ushiriki wa wananchi na idadi ya wagombea imekuwa kubwa, hii inathihirisha kuwa wananchi wamekuwa na uelewa mkubwa na wanatambua haki zao na kuitaka serikali iwajibike kwao.

Aidha Njoroge amezitaka tume za jumuia ya Africa Mashariki kufikiri kwa kina na kuweka mikakati ambayo itasaidia kupunguza gharama za Uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuandaa sera ya kusaidiana katika vifaa vya uchaguzi.

Viongozi hao wa Tume ambao wameitembelea Tanzania chini ya Mwenyeji wao ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja huo wa Tume za Uchaguzi za Jumuia ya Africa Mashariki na ndiye mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva walitembelea kitengo cha Daftari ambapo walijionea namna taarifa za Mpiga Kura zinavyoingizwa katika mfumo wa Daftari.

Wakiwa katika ziara hiyo Kamishna wa Tume huru ya Uchaguzi ya KenyaBalozi Mohamed Alawi ameipongeza Tume ya Uchaguzi ya Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanya kwa kuda mfupi imeweza kuandikisha wapiga Kura milioni ishirini na nne kwa kutumia BVR elfu nane (8,000) ukilinganisha na nchini mwake ambapo walikuwa na BVR 15,000 na waliweza kuandikisha wapiga Kura milioni kumi na tano kwa muda mrefu.Ikiwa ni pamoja na kuliweka wazi Daftari la awali la mpiga Kura mapema kuliko ilivyofanyika nchini kwao.

Aidha balozi Alawi aliongeza kuwa Uchaguzi ni zoezi kubwa katika nchi,haliwezi kuachiwa NEC pekeyake, kama inavyosemwa vita haiwezi kupiganwa na majemedali pekee, Uchaguzi ni zoezi linalofanywa na watanzania wote kwa ujumla, kwa maana hiyo ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wao wasitoe matamshi ambayo yatajenga chuki miongoni mwa jamii/ wapiga kura, tunafahamu watanzania ni wakomavu kisiasa, ni watu watulivu waitunze amani waliyonayo kwani Tanzania ipo kabla ya Uchaguzi, wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi.

Viongozi hao ambao wamekuja nchini kujiridhisha na maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa unaotarajia kufanyika mwezi ujao wa wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni kukemea vyama vya siasa vinavyokiuka maadili ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutoa matamshi ambayo yanaweza kujenga chuki miongoni mwa Watanzania.