Na dev.kisakuzi.com Kenya;
MATOKEO ya awali ya uchaguzi Mkuu nchini Kenya yameanza kutangazwa baada ya siku ndefu huku kura za awali zikionesha mchuano mkali upo kati ya Uhuru Kenyatta na kiongoza Raila Odinga. Hata hivyo hadi jana jioni Kenyatta kutoka muungano wa Jubilii alikuwa akiongoza kwa asilimia 54 huku mpinzani wake Odinga akimfuatia kwa asilimia 41.
Hata hivyo Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imewataka Wakenya kuwa watulivu na wavumilivu wakati wakiendelea na hatua za kutangaza matokeo hayo, imesema kwa sasa haitakiwi pande yoyote kushangilia au kunung’unika kwa kuwa matokeo hayo ni ya awali na hayawezi kutoa picha halisi ya matokero kwa sasa. IEBC imeanza kushtushwa na idadi kubwa ya kura kuharibika jambo ambalo halikutegemewa hapo awali.
Taarifa za mitandao ya kijamii baadae zilionekana kutoa taarifa kuwa mgombea Uhuru Kenyatta alikuwa akiongoza kwa kura 2,133,202 huku mwenzake Raila Odinga akimfuatia kwa kura 2, 718,021. Bado idadi ya kura zinaendelea kuhesabiwa hadi muda huu.