Uchaguzi DRC utata mtupu, waangalizi watofautiana

Mgombea aliyeshinda uchaguzi wa Congo uliozua vurugu na utata, Joseph Kabila

UJUMBE wa Kimataifa wa wasimamizi wa uchaguzi umetamka kuwa ni kweli uchaguzi uliofanywa katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ulikuwa na dosari kadhaa hivyo si wa kutegemewa.

Hata hivyo, tayari Rais Kabila alishinda katika uchaguzi huo. Kituo cha Carter kimesema kuwa uchaguzi huo umetiwa dosari, kwa kutotayarishwa sawasawa, na pengine ulikuwa na udanganyifu. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa matokeo ya vituo vya kupigia kura takribani 2000 mjini Kinshasa, ikiwa ni asilimia 20 ya vituo vya Mji Mkuu yalipotea.

Wajumbe wake wanasema takwimu rasmi za matokeo ya Jimbo la Katanga, Kusini mwa nchi, yanaonesha ulalamishi – maeneo mawili yalionesha kuwa Bwana Kabila alipata karibu kura zote. Kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi, ameyakataa matokeo rasmi yaliyotangazwa, na amejitangaza kuwa yeye ndiye rais.
-BBC