Ubabaishaji Wamkimbiza Mwandaaji Miss Tanzania Kanda Kaskazini

Mwaandaji wa shindano la Miss Kanda ya Kaskazini, Faustine Mwandago (kushoto.

Mwaandaji wa shindano la Miss Kanda ya Kaskazini, Faustine Mwandago (kushoto. 

Na Woinde Shizza, Arusha

MWANDAAJI wa Tamasha la Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni M
kurugenzi wa kampuni ya Mwandago Entertainment Ltd,Faustine Mwandago ametangaza kujiondoa rasmi kuandaa tamasha hilo huku akitaja sababu iliyompelekea ni pamoja na ubabaishaji uliojaa ndani ya mashindano hayo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa Mwandago alisema 
kwamba ameamua kuchana na kuandaa tamasha hilo kutokana na hali ya ubabaishaji iliyokithiri ndani ya mashindano hayo.

“Nimeamua kuachana na kuandaa tamasha hili kwa kuwa kuna mambo ya 
ubabaishaji mwingi ndani yake kadri ya siku zinavyokwenda
mambo 
yamekuwa na ubabaishaji sana umesikia hata Mwanza yaliyotokea yanakatisha tamaa,” alisema Mwandago

Alisema kwamba   mbali na sababu hiyo jambo jingine lililompelekea 
kuachana na uandaaji wa tamasha hilo ni pamoja na uhaba wa
wadhamini 
ambao umeshuka kwa kikubwa na kupelekea kudhohofisha mashindan0 hayo. Mwandago,alisema kwamba lakini pamoja na kuachana na kuandaa tamasha hilo atakuwa bega kwa began a mshiriki wa taji hilo kanda yaKaskazini katika safari yake na kumtaka mlimbwende huyo kutokuwa na wasiwasi.

“Pamoja na kwamba nimeamua kuachana na  kuandaa tamasha hili lakini 
mrembo anayewakilisha kanda ya kazkazini ambaye nilisimamia
uteuzi 
wake nitaendelea kumpa sapoti katika safari yake bila wasiwasi,” alisema Mwandago.