Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akieleza kwa ufupi kuhusiana na uzinduzi wa mashine za kutolea pesa za benki ya UBA ambapo Benki hio imezindua mashine hizo za kutolea pesa katika vituo vinne kwa hapa Dar Es Salaam
Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya UBA Tanzania, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma akikata utepe mbele ya Mashine ya kutolea pesa ya benki hiyo mapema leo katika uzinduzi wa vituo vya kutolea pesa vya benki hiyo.
Mkurugenzi wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akitoa pesa katika mashine ya kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya uzinduzi kufanyika katika kituo cha Mikocheni. Mashine hiyo ya kutolea pesa ya UBA bank ipo katika Kituo cha Mafuta cha Oilcom kilichopo Mbezi chini.
Mkurugenzi wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akisubiria pesa katika mashine ya kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya kuiamuru mashine kutoa pesa mara baada ya uzinduzi wa mashine hizo uliofanyika leo katika kituo cha Mafuta cha oilcom kilichopo mbezi chini
Mkurugenzi wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akichukua pesa katika mashine ya kutolea pesa ya benki ya UBA Tanzania mara baada ya kuiamuru mashine huku anayeshuhudia kushoto kwake akiwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Jenerali Mstaafu, Mh Robert Mboma.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo kumaliza kuzindua Mashine hiyo ya UBA Bank, uzinduzi uliofanyika leo Mbezi chini katika kituo cha mafuta cha Oilcom.
Mkurugenzi wa benki ya UBA Tanzania, Mh Peter Makau akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mwenyekiti wa bodi ya benki ya UBA Tanzania Jenerali Mstaafu Robert Mbona kumaliza kuzindua mashine hizo.
MWENYEKITI wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya UBA Tanzania, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma amezindua mashine nne za kutolea pesa za benki ya UBA katika kituo cha Mbezi chini huku uzinduzi huo ukiwa ishara ya kuzindua mashine nyingine tatu zinazopatikana katika maeneo ya Oilcom Mabibo, Oilcom Segerea, Oilcom Mbezi chini na Oilcom Mkuki Mall ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Uzinduzi wa mashine hizi umeenda sambamba na malengo ya benki hiyo ya kuhakikisha katika ukuaji wake inawasogezea huduma karibu wateja wake.
Akielezea katika UZinduzi huo Mkurugenzi wa Benki hiyo Hapa Tanzania, Mh Peter Makau amesema kuwa UBA benki ilikua na ndoto ya kusogeza karibu huduma zake huku lengo lao likiwa ni kuwa na mashine za kutolea pesa nje ya matawi yake na kwa kuanza tumeanza na Mashine za ATM nne ambazo zipo kwenye maeneo muhimu kama vile Oilcom Mabibo, Oilcom Segerea, Oilcom Mbezi chini na nyingine ndani ya jengo la manunuzi la Mkuki ambalo litafunguliwa hivi karibuni.
Vilevile Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo amesema kuwa aliruhusu kuanzishwa kwa mashine hizo za ATM kwaajili ya kuhakikisha inaendelea kukuza uchumi kwa Watanzania huku pia wakitarajia kufungua matawi mengine ndani ya Tanzania hivi karibuni.