
Wacheza show wa bendi ya Twanga Pepeta wakiwaburudisha mashabiki wao ndani ya Ukumbi wa Mango Garden jana Siku Kuu ya Idd jijini Dar es Salaam
BENDI maarufu ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta jana iliwaburudisha wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo katika onesho lililofanyika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ikiongozwa na waimbaji wake nyota na maarufu kama Chaz Baba, Sarehe Kupaza, Dogo Rama, pamoja na Muumini Mwinjuma aliyejiunga na bendi hiyo hivi karibuni-walikuwa ni kivutio kikubwa katika onesho hilo la Siku Kuu ya Eid. Zifuatazo ni picha mbalimbali zikionesha matukio katika onesho hilo.

Waimbaji maarufu wa Bendi ya Twanga Pepeta, Chaz baba (kushoto) na Mwinjuma Muumini (kulia) wakiwaburudisha wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo jana Ukumbi wa mango Garden.