‘Tuwafadhili wa Watoto Yatima Kielimu’

Rais Jakaya Kikwete akimpa zawadi mmoja ya wanamahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Nakayama.

Rais Jakaya Kikwete akimpa zawadi mmoja ya wanamahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Nakayama.

Na Magreth Kinabo – MAELEZO

RAIS Jakaya Kikwete ameitaka jamii kuwa na tabia ya kuwafadhili watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwenye elimu, chakula na malazi ili waweze kuendesha maisha yao kwa kujiajiri au kuajiriwa kwani kufanya hivyo ni kuimarisha nguvu kazi ya taifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Rais Kikwete wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari Nakayama inayomilikiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) iliyoko Nyamisati, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani.

Rais Kikwete aliwashukuru watu mbalimbali waliochangia shule hiyo kwa moyo wao wa upendo na huruma ili watoto wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira magumu  waweze kupata elimu, huku akisema kama wasi wafadhili hao isingekuwa rahisi watoto hao kuwezeshwa kusoma shuleni hapo.

“Mtapata fadhila kwa Mwenyezi Mungu kwa kila mtoto atakayesoma hapa…Mkopesheni Mwenyezi Mungu atawapa fadhila zake,” alisema Rais Kikwete.
 Kauli hiyo pia iliungwa na mkono na Mama Salma Kikwete ambaye alisema bila juhudi za pamoja kati ya Serikali, jamii na sekta binafsi watoto wengi wa kundi hilo watakosa elimu.

Shule hiyo inaendeshwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), ambapo Mwenyekiti wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Mama Kikwete alisema nchi ina Watanzania milioni 44.9 kama wapo wenye uwezo wapatao milioni tano kila mmoja akimchukua mtoto mmoja.

“Tanzania isiyokuwa na watoto wasio matumaini inawezekana,” alisema Mama Kikwete  huku akisema kwa kufanya hivyo kuwasaidia kujikwamua katika hali ya umasikini.
   
Rais Kikwete aliwataka wanafunzi hao kuwa na malengo ya kupata elimu ya juu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali na kulisaidia taifa, huku akisisitiza wawe jasiri kusoma fani ambazo wanawake wengi wanaogopa kuzisoma ambazo zitawawezesha kuwa mabingwa mafano udaktari, wahandisi na wanasheria.

“Hamna budi kushukuru na kujipongeza ombi langu ni kuweni watoto wema heshima na mabalozi wa shule hii. Shule hii itakapokamilika huduma zitakuwa bora. Shule hii ina kila sababu ya kuwa shule bora,” alisema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete alizitaka halmashauri nchini kuendelea kushishirikiana na Maendeleo (WAMA) kuwatambua watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata elimu kwa malengo ya taasisi hiyo.

Katika mahafali hayo Mwenyekiti wa kammpuni za IPP, Reginald Mengi aliahidi kuchangia shule hiyo Sh. milioni 200 kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano na Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (UWT) uliahidi kutoa Sh. milioni 10 yakiwemo mashirika mbalimbali yaliyoahidi kutoa michango  kadhaa.

Rais Kikwete katika mahafali hayo aliwatunuku vyeti wanafunzi 67 na kutoa zawadi za vyeti na fedha tasilimu kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri, ambapo mwanafunzi  aliibuka mshindi baada ya kufanya vema kwenye masomo ya biashara, historia na Kiingereza. Mwanafunzi aliyefanya vizuri kila somo alipata Sh. 100,000 na mwalimu Sh. 500,000. yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.