Kutoka kulia ni Meneja Mipango na Habari wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Nandi Mwiyombella, Meneja wa Kinywaji cha Tusker Sialuoise Shayo, Meneja Mipango na Ugavi wa SBL Kanda ya Ziwa, Dilip Chudasama na Meneja Mauzo wa Kanda, Octavian Migire (wa kwanza kushoto) kwa pamoja wakifanya uzinduzi rasmi wa Bia ya Tusker Lite Kanda ya Ziwa kwenye Hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.
Meneja wa Bia ya Tusker, Sialuoise Shayo akitoa ufafanuzi juu ya kinywaji hicho kwa wageni waalikwa wa hafla ya Uzinduzi wa Bia ya Tusker Lite Kanda ya Ziwa iliyofanyika Hoteli ya Golden Crest Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa idara ya masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakiwaonesha wageni waalikwa (hawapo pichani) chupa ya Bia ya Tusker Lite katika hafla ya uziduzi wa bia hiyo kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.
Kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Habari wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Nandi Mwiyombella, Meneja wa Kinywaji cha Tusker Sialuoise Shayo, pamoja na Meneja Mipango na Ugavi wa SBL Kanda ya Ziwa, Dilip Chudasama wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo.
Timu nzima ya mauzo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti kanda ya ziwa katika picha ya pamoja katika hafla ya uzinduzi wa bia ya Tusker Lite kanda ya ziwa iliyofanyika katika hoteli ya Golden Crest jijini Mwanza.