Mada mbalimbali zilitolewa na wataalamu wa masuala ya masoko kuwaongezea ujuzi wadau wa masuala ya masoko kutoka makampuni na taasisi anuai. Juu ni baadhi ya watoa mada wakizungumza na wageni waalikwa.
KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YADHAMINI USIKU WA WANATAALUMA WA MASOKO MAARUFU KAMA ‘MARKETER’S NIGHT’ KUPITIA BIA YAKE YA TUSKER LITE
KWA mara nyingine tena kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Tusker Lite imeendeleza umoja na mshikamano wa wanataaluma wa masoko na wafanya biashara mbalimbali jijini Dar es salaam ambapo wamekutana kwa lengo la kujiweka pamoja, kubadilishana mawazo na kukuza ushirikiano wao katika ufanyaji kazi na kujadili mustakabali mzima wa mazingira ya biashara katika kuhakikisha mambo yanaenda vizuri kibiashara.
Kwa namna ya kipekee hafla hiyo ilikuwa imesheheni makampuni na wajasiriamali mbalimbali. Usiku huo ulitawaliwa na burudani kabambe, chakula kizuri na kikubwa zaidi ni hotuba mbalimbali zenye mafunzo kwa wanataaluma hawa ziliotolewa na watoa mada mbali mbali. Mtoa mada mkuu katika hafla hiyo alikuwa Bw. Loan Carpus, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Six Paths Consulting. Pia mada nyngine ilitolewa na Bw. Charles Makulu, mkurugenzi wa Ipsos Synovate ambapo mada hiyo ilizungumzia suala la “utafiti katika masoko katika ulimwengu wa digitali”.
“Kampuni ya bia ya Serengeti imewekeza kwa kiasi kikubwa mikakati inayolenga kupanua wigo wa kibiashara na kukutananisha makampuni na wafanyabiashara mbalimbali katika kuhakikisha biashara zinaboreshwa na kuendeshwa kisasa. ‘Marketers night’ ni mojawapo ya jitihada ambazo zinafanikisha malengo hayo. Bila shaka wanataaluma wa masoko wameweza kujipatia fursa adimu na kujifunza kutoka kwa mifano hai kupitia kwa watoa mada wetu usiku wa leo.” Alisema Bi Sialouise Shayo, Meneja wa bia ya Tusker Lite.
“Tumekuwa wadhamini wakuu wa usiku huu kwa mwaka wa tatu sasa. Kuwa pamoja nao kumetupatia fursa kubwa ya kujumuika pamoja na kufurahia bia waipendayo ya Tusker lite, ambayo kwa kiasi kikubwa inaendana na maisha yetu”, Aliongeza Bi Shayo.
Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako. Haiuzwi kwa walio chini ya miaka 18.
Kampuni ya bia ya Serengeti inajihusisha na biashara ya vinjwaji vyenye vileo kama bia- Premium Serengeti Lager, Tusker Lager, Tusker Malt Lager, Uhuru Peak Lager, Pilsiner, Guinness na vinywaji vikali kama Johnnie Walker, Smirnoff Vodka, Richot, Bond 7 and Gilbeys. Pia vinywaji visivokuwa na kileo kama Malta Guinness na Alvaro.
Serengeti Breweries Limited ni kampuni tanzu ya EABL/ DIAGEO. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Mkurugenzi wa mawasiliano na uhusiano Bw. Evans Mlelwa: Evans.Mlelwa@diageo.com