Kinana alisema CCM haina hofu na uchaguzi maana inakwenda kushindana na makapi yake ambao ni watu walioshindwa uchaguzi ndani ya chama na kukimbilia vyama vingine. “…Tunaenda kushindana na makapi yetu ni lazima kushinda, kwasababu tunashindana na makapi,” alisema Katibu Mkuu huyo wa chama tawala.
Magufuli na mgombea mwenza, Bi. Suluhu wamechukua fomu rasmi za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo majira ya saa sita mchana katika msafara mkumbwa ukiongozwa na umati mkubwa wa wanaCCM waliojitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea wao hadi ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi na baadaye shughuli hiyo kupokelewa yalipo makao makuu ya ofisi za CCM mtaa wa Rumumba jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafka hivyo, Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais wa Tanzania alisema chama hicho kina kila sababu ya kujidai kwani kimefanya maendeleo makubwa katika uongozi wake kikiwa madarakani mambo ambayo hata jumuiya za kimataifa zinayatambua. Alisema CCM inasifa na uzoefu mkubwa wa kuendesha dola hivyo inakila sababu ya kushinda Uchaguzi Mkuu na itawashinda wapinzania wake kama wamesimama.
“…Yaani kama ni mpira wa miguu tutafunga magoli wao wakiwa wamesimama…Tumejiandaa vya kutosha kushinda na kushinda tutashinda, tunao uzoefu, tunayo maarifa na uwezo wa kushinda tunao,” alisema huku akishangiliwa na wanaCCM.
Hata hivyo aliwataka wanaCCM wasimdharau adiu kwani aduni ni adui hata akiwa mdogo, hivyo kuwataka kushirikiana katika kuelekea uchaguzi kuhakikisha chama kinapata kura za kutosha. Aliongeza kuwa CCM imejipanga kwa hoja na ina mengi ya kuzungumzia uzuri wa chama hicho. “…Nchi ni tulivu, maendeleo yanaonekana na dunia nzima inajua tumepata mafanikio sasa kwanini CCM isishinde,” alihoji Rais Kikwete na kuendelea kuwa nchi ina demokrasia na utawala bora pamoja na uhuru wa vyombo vya habari.
Akizungumza katika hadhara hiyo Dk. Magufuli aliwashukuru umati wa watu na wanaCCM waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu na kuwaahidi amejiandaa kuwatumikia bila kujadi itikadi zao, alisema yeye pamoja na mgombea mwenza anautambua ushirikiano huo. Alikishukuru chama cha CCM kwa kumuamini na kumteuwa kupeperusha bendera ya chama hicho.
Alisema mkusanyiko wa watu waliojitokeza kwenye hafla hiyo na msafara mzima ni ushahidi tosha kuwa chama hicho kitaendelea kuwa madarakani. Leo ilikuwa ni siku ya kuchukuwa fomu na nyinyi mmeshuhudia tumechukuwa na tutaizungusha kupata wadhamini kama ilivyo elekeza,”
Alisema shida za watanzania anazijua na matatizo ya Watanzania anayajua hivyo haita kuwa ngumu kufanya kazi yake na ukizingatia msingi mzuri uliowekwa na chama chake hivyo ni dhahiri CCM ina kila sababu ya kuendelea kuwa madarakani. Aliongeza kuwa anamengi ya kusema kwa wananchi lakini wakati wa kampeni bado hivyo wakati ukifika atazungumza.
CCM inatarajia kuzinduwa kampeni zake Agosti 22 jijini Dar es Salaam na tayari kuanza kazi ya kuinadi ilani ya chama na wagombea wake.