Tume ya Uchaguzi Yatoa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi kwa vyombo vya habari.

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi kwa vyombo vya habari.


Na Mwandishi Wetu

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imetangaza rasmi ratiba ya Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2015. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Jaji wa Rufaa Damian Lubuva uteuzi wa nafasi za wagombea unatarajiwa kuanza Agosti 21, 2015 vyama vyote vya siasa.

Taarifa hiyo imesema uteuzi wa nafasi hizo ni pamoja na Wagombea Urais, Ubunge na nafasi za madiwani kwa vyama. Taarifa hiyo imesema kampeni za uchaguzi zitaanza rasmi Agosti 22 hadi 24 Oktoba, 2015.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuviarifu vyama vya siasa na Wananchi wote kwa ujumla kuwa kwa mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35 B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46(1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Ratiba ya Uchaguzi Mkuu itakuwa kama ifuatavyo:-…” imeeleza taarifa hiyo kama ilivyotajwa juu.

Taarifa hiyo imesema siku ya kupiga kura itakuwa ni Oktoba 25, 2015 ambapo raia wote wenye sifa wataruhusiwa kutimiza haki yao kikatiba. KUtolewa kwa ratiba hiyo ya uchaguzi ni kipenga kwa vyama vya siasa kuanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi huo.