Tuhuma za Rushwa FIFA, Interpol Yakamata Vigogo Sita

Tuhuma za Rushwa FIFA, Interpol Yakamata Vigogo Sita

Tuhuma za Rushwa FIFA, Interpol Yakamata Vigogo Sita


SHIRIKA la Maofisa wa Polisi wa Kimataifa, Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi. Agizo hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.

Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita. Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe, lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.

Afrika kusini imekana kwa mara nyengine tena kwamba ilitoa hongo ili kupewa maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2010. Waziri wa michezo nchini humo Fikile Mbalula, amewaambia wanahabari kwamba Afrika kusini itashirikiana na wachunguzi kutoka Marekani lakini imekataa kuingizwa katikati ya ugomvi kati ya FIFA na Marekani.

Alisema kuwa dola millioni 10 zilizotolewa zilikuwa malipo ya kusaidia soka miongoni mwa raia wa Afrika wanaoishi katika visiwa vya Caribbean na yalilipwa miaka kadhaa baada ya michuano hiyo kuandaliwa na Afrika kusini.
-BBC