Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.
Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.
Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake. Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu
Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.