TTCL Yazinduwa Promosheni Mpya Ya ‘Bwerere’

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Bwerere iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Bwerere iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa TTCL na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa promosheni mpya inayojulikana kama Bwerere.

Mkutano wa TTCL na waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa promosheni mpya inayojulikana kama Bwerere.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika uzinduzi rasmi wa promosheni mpya inayojulikana kama Bwerere.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika uzinduzi rasmi wa promosheni mpya inayojulikana kama Bwerere.

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu nchini (TTCL) imezinduwa rasmi promosheni mpya kwa wateja wake wa majumbani na maofisini ambao wanatumia huduma ya malipo kabla (pre-paid). Katika promosheni hiyo inampa mteja gharama za viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na wenyewe wa TTCL.

Akizinduwa huduma hiyo leo jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Peter Ngota alisema promosheni hiyo kabambe inayolenga kuwapa fursa wananchi huduma bora na za bei nafuu katika kufanya mawasiliano kukidhi mahitaji ya wateja.

“…Siku ya leo, TTCL inazindua rasmi promotion inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la BWERERE yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi,” alisema Ofisa huyo Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL.

Akifafanua zaidi alisema kuwa promosheni hiyo inatoa fursa kwa wateja wa majumbTani na maofisini ambao wanatumia huduma ya malipo ya kabla kufurahia gharama za viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda mitandao mingine yote pia pamoja na TTCL yenyewe.

Aidha Ngota alisema katika promosheni hiyo pia inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA) kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo wa TTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo.

Alisema katika promosheni hiyo pia mteja atapata fursa ya kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa shilingi 1 kwa sekunde na huduma hii haina kujiunga, ilhali hapo awali huduma ilikuwa ikigharimu shilingi 230 kwa dakika 1.

“…Kwa sasa mteja wa TTCL ataweza kupiga simu katika mitandao mingine na kuweza kuongea na ndugu, jamaa na marafiki kwa Tsh 1 moja kwa sekunde yaani kwa gharama ya shilingi sitini kwa dakika 1; Sawa na punguzo la Asilimia zaidi ya asilimia 70,” alisema.

Alizitaja huduma zingine ni ‘Bwerere Premium’ inayohusisha wateja wanaotumia huduma ya intaneti kuanzia kiwango cha 2Mbps mpaka 32 GB kutapata fursa ya kupiga simu kwenda TTCL bure ndani ya mwezi, pia mteja atapata muda wa maongezi kuanzia dakika 300 mpaka dakika 600 kupiga simu kwenda mitandao mingine ndani ya mwezi.

Ngota alisema huduma nyingine ni ‘Bwerere Unlimited’ inayohusisha watumiaji wa intaneti kuanzia kiwango cha 512Kbps mpaka 2Mbps watapata huduma ya muda wa kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL kwa muda wa mwezi mzima. Nyingine ni ‘Bwerere’ kwa watumiaji wa intaneti njia ya Broadband kuanzia 3 GB mpaka 24 GB inayotoa fursa ya kupiga simu bure TTCL kwenda TTCL.

“…Ninayo furaha kubwa katika siku hii ya pekee kuujulisha umma kuwa TTCL inatoa fursa kwa wateja wake na umma kwa ujumla kutumia mtandao wa TTCL kupata huduma ya mawasiliano BORA ya simu na intaneti kwa bei nafuu zaidi. Tunaendelea Kupanua wigo wa uchaguzi wa huduma za vifurushi kwa watumiaji na kuwapa fursa ya Watanzania kutumia huduma za TEHAMA kwa bei nafuu kwa maendeleo ya M-Tanzainia na Taifa,” alisema Ngota.

Akizitaja faida za simu za mezani, ofisa huyo alisema simu za mezani zinausalama mkubwa kwani sio rahisi mtu kuingilia mawasiliano ambayo yanatolewa kwa njia ya waya (cable) na ni nzuri kwa matumizi ya kiofisi na majumbani, kutokana na urahisi kutambua sehemu ya ofisi au nyumba unayoishi, mbali na kuthibitisha uwepo wa mtu unayewasiliana naye katika eneo husika.

Hata hivyo, aliongeza kuwa simu za mezani mawasiliano yake yana ubora mkubwa na uhakika kiusikivu huku ikiwa na kasi zaidi kwa matumizi ya intaneti. “…TTCL ni kampuni pekee hapa nchini ambayo inatoa huduma za DATA, simu zenye ubora zaidi. Ni mtandao pekee ambao umeenea katika mikoa na wilaya zote nchini. Sasa ni wakati mzuri wa kutumia na huduma hii ya BWERERE na Ufaidike zaidi na TTCL kwa UBORA wa huduma na gharama nafuu zaidi nchi nzima,” aliwaeleza wanahabari hao.