Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’.
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’ wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.

Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa kwa mmoja wa walezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’.
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’ wakiteremsha sehemu ya msaada uliyotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.
Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’. Kushoto ni MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza.
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’ wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.
Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la ‘Yatima Group Trust Fund’ wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.
Picha ya pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi baada ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kukakabidhi sehemu ya msaada kwa watoto hao jana jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa zawadi ya Siku Kuu ya Pasaka kwa kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa ‘Yatima Group Trust Fund’.
TTCL imekabidhi msaada huo wa mchele kilo 150, maharage kilo 100, unga sembe kilo 125, mafuta ya kula ndoo nne, maji katoni 25, juisi katoni 15 pamoja na chumvi mifuko 2 jana kituoni hapo na kupokelewa na MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo aliziomba taasisi anuai na jamii kwa ujumla kuwakumbuka yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa kipindi hiki cha siku kuu ambapo nao wangependa kufurahi pamoja.
Alisema jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wengine waliopo katika mazingira hatarishi si kazi ya vituo vilivyojitolea au serikali tu bali kila mwanajamii hasa wale wenye uwezo.
Alisema TTCL itaendelea kuyakumbuka makundi anuai yenye uhitaji kila ipatapo nafasi kwani hilo ni moja ya jukumu lao kurejesha sehemu kidogo kwa jamii kwa njia ya kusaidia popote, kwani wao ni sehemu ya jamii.
“…Kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kamugisha Kazaura na wafanyakazi wote napenda kutoa msaada huu wa vyakula kwa ajili ya kituo chako cha kulelea watoto yatima katika kuelekea katika sherehe za siku kuu ya Pasaka,” alisema Matondo akikabidhi msaada huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Yatima Group Trust Fund, Lubanza aliishukuru TTCL kwa moyo huo wa kujitolea kwa kuwakumbuka watoto wanaolelewa katika kituo hicho hasa kipindi hiki cha siku kuu ya pasaka.
Alisema wanafarijika sana wanapoona jamii na taasisi mbalimbali zikishiriki kuwasaidia watoto yatima na wengine walio katika mazingira hatarishi kwani ishara hiyo ni kuonesha kila mmoja anawajibika katika suala hilo ambalo ni changamoto kubwa nchini.