TTCL Yakanusha Taarifa ya Gazeti la The East African

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba.

TAARIFA KWA UMMA

KAMPUNI YA SIMU TANZANIA TTCL, INAPENDA KUUJULILISHA UMMA KUWA,TAARIFA ILIYOCHAPISHWA KATIKA UKURASA WA MBELE WA GAZETI LA THE EAST AFRICAN TOLEO NAMBA 1158 LA TAREHE 07-13 JANUARI 2017 KUHUSU TTCL KUONGEZEWA MUDA WA KUJIUNGA NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM SIO SAHIHI. TTCL KAMA ZILIVYO KAMPUNI NYINGINE ZA MAWASILIANO, INAWAJIBIKA KUTEKELEZA SHERIA NA MAELEKEZO YA SERIKALI PASIPO KISINGIZIO CHOCHOTE NA IMEKUWA IKIFANYA HIVYO KILA MARA KUNAPOKUWA NA MAELEKEZO YANAYOHITAJI UTEKELEZAJI.

TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWETU NI KUWA, TTCL INATEKELEZA KIKAMILIFU SHERIA INAYOTUTAKA KUJIUNGA NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM NA TAYARI TUMESHAWASILIANA NA MAMLAKA HUSIKA NA KUCHUKUA HATUA KADHAA ILI KUTEKELEZA KIKAMILIFU TAKWA HILI LA KISHERIA. PAMOJA NA TAARIFA HII KWA UMMA,

TUNAENDELEA KUWASILIANA NA UONGOZI WA GAZETI HUSIKA ILI KUREKEBISHA KASORO ZILIZOJITOKEZA KATIKA TAARIFA YA GAZETI LAO TOLEO TAJWA HAPO JUU NA KUANDIKA KWA USAHIHI TAARIFA HII KWA KUZINGATIA MISINGI YA TAALUMA YA UANDISHI WA HABARI.

IMETOLEWA NA,
WAZIRI W. KINDAMBA KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU- TTCL 10 JANUARI, 2017