TTCL Kupeleka Mawasiliano Katika Vijiji 76

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akitoa hotuba yake kwenye hafla ya kusaini mikataba kati ya UCSAF na Makampuni ya Simu kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini.

6. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akitoa hotuba yake kwenye hafla ya kusaini mikataba kati ya UCSAF na Makampuni ya Simu kwa ajili ya kupeleka mawasiliano vijijini.

Ofisa Mtendaji wa TTCL Dk. Kamugisha Kazaura akisaini mkataba pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Ulanga huku wakishuhudiwa  na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa.

3. Kaimu  Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Prof. John Nkoma akihutubia kwenye hafla kusaini mikataba ya kupeleka mawasiliano vijijini pamoja na makampuni ya simu.

Katibu Mkuu wa Wazira ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Ngodo akihutubia katika hafla kusaini mkataba wa kupeleka mawasiliano vijijini na Makampuni ya Simu.

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa UCSAF Mhandisi. Peter Ulanga akihutubia kwenye hafla ya kusaini mkataba wa kusambaza mawasiliano vijijini na makampuni mbalimbali ya simu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma akizungumza katika hafla ya katika hafla ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kusaini mkataba na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imesaini mkataba na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye gharama ya USD 2,244,376/- milioni (sawa na Tsh 4.1/- bilioni) kwa ajili ya kupeleka mawasiliano ya simu katika kata 19, yenye vijiji 76.

Kata hizo zinatakazonufaika na mradi huu ni pamoja na; Gelai Meirugoi, Arash na Olbalbal- Arusha, Mbondo – Lindi, Makame Shambarai na Masieda- Manyara. Kata nyingine ni pamoja na Ivuna – Mbeya, Masagati na Mombo- Morogoro, Vikumbulu- Pwani, Ligera. kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma zipo kata ya Lukumbule, Marumba, Nakapanya na Nampungu. Aidha kwa mkoa wa Singida zipo kata za Minyughe na Urughu, mwisho kata ya Ubangaa iliyopo mkoa wa Tanga.

Mkataba ambao leo unasainiwa rasmi, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) itatoa huduma za kawaida za mawasiliano ya simu yaani maongezi na huduma za ujumbe mfupi (SMS) na Intaneti.

Mradi huu utakapokamilika, utaleta chachu ya ukuaji wa wa maendeleo katika kata hizo ikiwa ni pamoja na; wananchi wataweza kuwasiliana na pande zote za dunia, kupata na kutumia taarifa za kibiashara, kupata habari za masoko mapya na za kijamii.

Aidha, huduma hii itawawezesha kutoa fursa sawa na watu wa maeneo ya mijini ili kuendelea kujenga uwiano sawa wa kupata na kutoa taarifa kwa maendeleo ya jamii.