TRUMARK Yaja na Warsha Maalum Siku ya Wanawake Duniani

Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza  jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.

Mratibu wa Warsha hiyo Antu Mandoza (kulia), akisisitiza
jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa warsha hiyo, Nuru Lyau.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu warsha maalumu iliyoandaliwa na kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika Machi 7, 2015 ukumbi wa Mlimani City. Wengine kutoka kushoto ni maofisa wa Trumark,  Antu Mandoza na Nuru Lyau.
Na Dotto Mwaibale
 
KAMPUNI ya TruMark ya jijini Dar es Salaam imeandaa warsha yenye lengo la kumjengea mwanamke uwezo wa kutambua changamoto na kuzigeuza kuwa fursa.
 
Hayo yamemwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Agness Mgongo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Mgongo alisema warsha hiyo itafanyika Machi 7, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa  Mlimani City ikiwa ni siku moja kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
 
‘Tunataka tumjengee mwanamke uwezo wa kujiamini, kujithamini na kutambua kuwa changamoto anazozipata ni fursa zitakazomfanya aweze kupambana na makali ya maisha na kisha kujiendeleza bila kumtegemea mwanaume’ alisema Mgongo.
 
Aidha Mgongo alisema kuwa warsha hiyo itajumuisha shuhuda na maonesho ya bidhaa na kazi za mikono kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kupitia changamoto mbalimbali walizozipitia.
 
‘Siwezi kuwataja ila watakuwepo wanawake ambao walikumbwa na changamoto mbalimbali lakini hawakukata tamaa na mwisho wa siku wakafanikiwa,’ alisema Mgongo.
 
Naye kwa upande wake Mratibu Mkuu wa warsha hiyo, Antu Mandoza alisema kuwa kutakuwa na kiingilio cha sh. 50,000 ambayo asilimia 10 ya fedha zitazopatikana zitaelekezwa katika kuwaandaa wasichana kujitambua mapema kabla ya kuingia katika soko la ajira.
 
‘Tutaenda katika shule mbalimbali za wasichana kuwafundisha mbinu nbalimbali za kuwa wajasiriamali na kujiajiri punde wanapohitimu masomo yao’ alisema Mandoza.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)