TPLB Yampongeza Nape Kuwa Wazuri wa Michezo.

nnauye-607x360
Mwenyekiti wa Bodi ya TPLB Yahya Hamad amesema kwa Bodi hiyo inapenda kutoa pongezi za jumla kwa uongozi imara wa nchi yetu, uliofanikisha kukamilisha uchaguzi mkuu, ambapo Mhe. John Pombe Magufuli.

Amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunampongeza sana na pia kumshukuru Mhe. Rais, kwa kumteua Mhe. Nape Nnauye (MB) kuwa Waziri wa Wizara inayohusika na michezo.

“Tumefarijika sana kumpata kijana mwenzetu na tunaimani atakua mchango mkubwa katika kuendeleza Michezo, hasa Mpira wa Miguu” alisema Hamad
caflicence
Bodi imeendesha Ligi Kuu ya mwaka jana ambapo timu ya Yanga walitawazwa kuwa mabingwa, na vile vile imeendesha Ligi Daraja la Kwanza ambapo klabu tatu zilipanda daraja, na kwa mwaka huu, pamoja na kuendesha ligi hizo mbili

Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeiomba Bodi pia iendeshe Ligi Daraja la Pili ambayo inaendelea hadi sasa.