Na Mwandishi Wetu
OGANAIZESHENI ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) imetangaza kujitoa katika mpambano wa ngumi kati ya mabondia Selemani Saidi na Caled Ameinda baada ya kudai muandaaji wa mpambano huo ameshindwa kutimiza masharti kabla ya pambano hilo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa TPBO, Yassin Abdallah Mwaipaya kwa vyombo vya habari, chama hicho kimeamua kujitoa baada ya kuona muandaaji wa pambano, Yusuph Montanga (GACHA) anashindwa kutimiza masharti.
“Napenda kuwaarifu kwamba TPBO haihusiki na pambano la ngumi za kulipwa kati ya mabondia waliotajwa hapo juu. TPBO inalazimika kutoa taarifa hii kutokana na masharti iliyompatia muandaaji wa pambano hilo GACHA kushindwa kuyatekeleza.
Pia izingatiwe kwamba TPBO ilitoa kibali kwa muandaaji (GACHA) kwa ajili ya pambano kati ya bondia THOMAS MASHALI VS SELEMANI SAIDI ambalo lilitakiwa kuchezwa katika uwanja wa KINESI ulioko katika Jimbo la Ubungo Novemba 10, 2012.”
“…Lakini kokana na kuumia kwa bondia THOMAS MASHALI katika pambano lake la kugombea ubingwa wa AFRIKA MASHARIKI NA KATI dhidi ya bondia kutoka uganda MEDI SEBYALA, tpbo ililazimika kumsaidia muandaaji huyo ndg GACHA ili aweze kumpata bondia kutoka kenya ili awe mbqdala wa THOMAS MASHALI,” alisema Mwaipaya katika taarifa yake.
Akielezea zaidi Mwaipaya alisema; “…TPBO ilianza mawasiliano na kocha Juliusn Odhiambo kutoka Kenya ili atupatie bondia wake. Lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele TPBO ilipata wasiwasi na uwezo wa muandaaji huyo kuweza kuandaa pambano hilo hasa alipofikia kutopokea simu ya RAIS wa TPBO kuhusu maendeleo ya maandalizi ya pamnao hilo.
“Novemba 5, 2012 nilimuagiza ndg GACHA alete pesa za kuwasafirisha bondia na kocha wake kutoka kenya ili wawasili nchini siku ya alhamisi usiku kwa ajili ya zoezi la upimaji wa uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya pambano la Novemba 10, 2012 kama kanuni ya ngumi za kulipwa zinavyoamuru, upimaji wa uzito kwa mabondia siku moja kabla ya pambano.”
“Na ikafikia hata mimi kumpatia GACHA namba za simu za ndg bakari ambaye ni mfanyakazi wa SPIDER BUS SERVISES ili awasiliane naye kuhusu ujio huo wa bondia kutoka kenya. lkn mpaka hivi sasa ninapoandika taarifa hii kwenu sijapata taarifa yoyote inayohusu kuwasili kwa mabondia hao kutoka kenya na hivyo TPBO haiwezi kuvnja kanun i za mchezo wa ngumi za kulipwa, kwa kumfurahisha tu MUANDAAJI.”
TPBO pia ilimpa masharti GACHA awasilishe TPBO pesa za kuwarudisha wakenya baada ya mchezo badala ya kutegemea makusanyo ya mlangoni, pia awasilishe DOLA 100 ambayo ilikuwa ni malipo ya bondia huyo kutoka kenya kabla ya pambano, lakini alikataa. Kwa taarifa hii TPBO inatamka rasmi kwamba isihusishwe na lolote litakalotokea endapo bondia huyo kutoka kenya atakuwa amewasili kwa njia zingine ambazo NDG GACHA atakuwa ameamuwa kuzitumia.
TPBO inalazimika kutowa taarifa hii kwenu ili kulinda heshima yake na uaminifu ambayo imejijengea katika nchi nzima ya tanzania na haiko tayari kufanya kazi na waandaaji ambao uwezo wao ni wa kujaribu jaribu mambo na siyo wazoefu kwani hatimaye huwa ni kuuvunjia heshima mchezo wa ngumi za kulipwa na kusababisha udharauliwe.
Wakati TPBO ikijitoa katika pambano hilo, maandalizi ya mpambano kati ya mabondia hao yaani SELEMANI SAIDI na CALED AMAEINDA yanaendelea na pambano linatarajia kuchezwa kesho katika uwanja wa KINESI ulioko Ubungo. Akizungumza na vyombo vya habari Rais wa PST, Emanuel Mlundwa amethibitisha kuwepo kwa mpambano huo ambapo CALED AMAEINDA wa Kenya tayari amewasili kwa ajili ya mpambano na Seleman siku iliyopangwa.
Alisema taarifa zilizotolewa na TPBO imewakera hivyo wao kuamua kuingilia kuchukua jukumu la kukwamua ili kufanyika mpambano huo na lengo kubwa ni kuhakikisha mabondia wapate ridhiki yao ya alali kama walivyokubaliana katika mkataba. Mlundwa alisema mabondia ndio wanaopigana hivyo hana sababu ya kusitisha mpambano huo kwa baadhi ya watu wachache wasioutakia mema mchezo wa masumbwi kuleta fujo za uongozi wa hapa na pale.
Mpambano huo utakuwepo pale pale kesho kuanzia saa kumi jioni na kuendeklea na baadhi ya wachezaji wanaocheza utangulizi wamepima uzito leo kwa ajili ya mpambano huo na kuwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia masumbwi hayo