Tovuti ya Modewjiblog Yavuta Wengi Sabasaba…!

Pichani ni Meneja Mwendeshaji wa tovuti ya Modewjiblog, Zainul Mzige akiwapa ufafanuzi wadau waliotembelea banda la tovuti hiyo lililopo MeTL Pavillion katika maonesho ya kimataifa ya kibiashara ya Sabasaba yanayoendelea katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Bw. Zainul pia ametumia fursa hiyo kutaja umri wa tovuti hiyo ambapo amesema sasa inatimiza miaka saba (7) tangu ilipoanzishwa na kuwa inatarajia kuadhimisha “birthday” itakapofika mwezi wa tisa mwaka huu na amewataarifu wadau kukaa mkao kujiachia.

IMG_6930

Tovuti mahiri ya habari ya modewjiblog leo imevuta umati wa watu wanaotembelea maonyesho ya 39 ya kimataifa ya kibiashara Sabasaba katika banda lake lililopo MeTL Pavillion.

Wengi kati ya watu hao walikusanyika kutaka kujua ni jinsi gani tovuti inavyofanyakazi kwa haraka na usahihi sambamba na picha za matukio yanayokuwa yamejiri kwenye habari husika.

Akitoa maelezo kwa kina Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Bw. Zainul Mzige amesema ni kutokana na uelewa wa watendaji wa tovuti hiyo na kujituma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla.

Akitoa maoni yake wakati alipotembelea banda la Modewjiblog, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema amesema anafurahishwa sana na habari zinazoandikwa na tovuti hiyo na kuwa yeye ni mdau mkubwa kwani kila siku lazima aitembelee ili kujua dunia inaendaje.

Aidha tovuti hiyo imewataka watu wafike katika maonyesho hayo kutembelea katika banda lake ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali wanayotaka kujua kuhusu Modewjiblog na pia kutoa maoni yao.

IMG_6931

IMG_6906

IMG_6954

IMG_7196

Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian, akisimamia zoezi la wadau kutia saini kwenye kitabu cha wageni.

IMG_6983

Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian akitoa kipeperushi kwa wadau waliotembelea banda letu.

IMG_6902

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Modewjiblog katika maonyesho ya sabasaba. Kwa matukio zaidi ya picha bofya link hii