Toure Ashinda Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika.

151211154640_yaya_toure_afoty_512x288_bbc_nocredit
Yaya Toure Raia wa Ivory Coast ameshinda tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2015, baada ya kuwashinda Yacine Brahimi, Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew na Sadio Mane.

Mchezaji huyo wa kati wa Klabu ya Manchester City mwenye umri wa miaka 32 anakuwa mwanasoka wa tatu, baada ya Wanigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha, kushinda tuzo hiyo mara mbili, mara ya kwanza ilikua mwaka 2013.

Brahimi kutoka Algeria ndiye aliyeshinda tuzo hiyo mwaka jana naye Mghana Ayew aliishinda 2011. Aubameyang kutoka Gabon alikuwa akishindania tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mtawalia, huku Mane, kutoka Senegal, akishindania kwa mara ya kwanza.

Toure ameteuliwa kushinda tuzo hii mara sita na ushindi wake mara hii unahakikisha anafunga mwaka akiwa na tuzo kuu, sawa na alivyouanza kwa kuongoza Ivory Coast kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwezi Februari mwakani.

Lakini Toure amesalia kuwa nguzo katika safu ya kati na amechangia katika ufungaji wa mabao saba kwa klabu yake mwaka huu.
Washindi wa zamani wa Tuzo ya BBC
2014: Yacine Brahimi (Porto & Algeria)
2013: Yaya Toure (Manchester City & Ivory Coast)
2012: Chris Katongo (Henan Construction & Zambia)
2011: Andre Ayew (Marseille & Ghana)