Toto Yaharibu Hesabu za Simba Taifa

Nembo ya Simba

Klabu ya Simba imefungwa bao 1-0 na Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waziri Junior ndiye aliyefunga bao hilo pekee dakika ya
20 kwa shuti kali la umbali wa mita 20 lililomshinda kipa Muivory Coast, Vincent Angban.

Simba inayobaki na pointi zake 57 baada ya kucheza mechi 25, inaendelea kuwa nafasi ya pili, mbele ya Azam FC yenye pointi 55 za meci 24, wakati Yanga wenye pointi 59 za mechi 24 wapo juu.