TNRF Wamtaka Dk Magufuli Adhibiti Upotevu wa Maliasili Tanzania

 Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini (TNRF) ,Dr.Suma Kaare akizungumza katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili. 

  Mkurugenzi wa Shirika la Haki kazi Catalyst Alais Moridant akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

  Mkurugenzi wa Shirika la AWF ,John Salehe akifafanua jambo  katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

  Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

  Viongozi mbalimbali wa jumuiko la maliasili wakiwa katika mkutano wa 7 wa jumuiko hilo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha wakiwa katika picha ya pamoja, ,mkutano huo ulihudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

Mwakilishi wa Shirika la WWF ,Sware Semesi  akizungumza katika  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini
Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

 Washiriki wa  mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

Wasemaji Wakuu wa mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na mashirika binafsi pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya maliasili.

Mwenyekiti wa Jumuiko la Maliasili nchini Dr.Suma Kaare amemtaka Raisi John Pombe Magufuli adhibiti upotevu wa mali asili za wanyama pori na misitu uliokithiri katika maeneo mengi nchini ili kunusuru uhai wa maliasili.
Suma Kaare amesema  hayo katika mkutano wa 7 wa jumuiko la maliasili  unaoendelea jijini Arusha,Kaare amesema kuwa jukwaa hilo litashirikiana na Rais huyo katika  kuhakikisha kuwa maliasili zinalindwa na kuwanufaisha Watanzania kwa kiwango stahiki.

“Tunajua Rais wetu mpya ana kazi  kubwa  ya kulinda maliasili za nchi hii kama ilivyo kauli mbiu yake ya “kazi tu” tunaamini atazuia upotevu mkubwa wa rasilimali unaofanywa na watendaji wasio waaminifu” Alisema Kaare Mratibu wa Masuala ya misitu katika shirika la uhifadhi wa maliasili na Mazingira (wwf), Isaac Malungu amesema kuwa asilimia 90% ya nishati inayotumika nchini inatokana na kuni pamoja na mkaa hali ambayo inaathiri misitu na kutishia uhai wa maliasili nchini hivyo ameitaka serikali ihimize matumizi ya nishati mbadala ili kunusuru mazingira yanaoharibiwa kila kukicha.
Malungu alisema kuwa kilimo cha kuhama hama pamoja na ukataji miti ovyo umekua ukisababisha uharibifu wa mazingira na hata kupelekea hecta laki 4 za misitu kupotea kila mwaka kutokana na shughuli hizo.
Mkurugenzi wa  Shirika la AWF,John Salehe Alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yamesababisha hali ya ukame inayowaathiri
wanyama pamoja na mimea hivyo kuathiri uhifadhi kwa ujumla. 
Salehe alisema kuwa juhudi zaidi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo upandaji wa miti pamoja na kutunza misitu ili kurejesha uoto wa asili uliopotea.
Chanzo; Wazalendo 25 Blog