TIMUATIMUA iliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wake mkuu maalum mjini Dodoma imemkumba Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba (Mb), na wenyeviti wa CCM Mikoa ya Dar es Salaam (Ramadhani Madabida), Iringa (Jesca Msambatavangu) , Shinyanga (Erasto Kwilasa), Mara (Christopher Sanya) na wenyeviti wa CCM wilaya.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema adhabu hiyo imetolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kile wanachama hao baada ya kupatikana na makosa ya maadili kinyume na katiba ya CCM.
Taarifa imeonesha mbali na waliofukuzwa wapo waliopewa onyo kali na kuzuiwa kutogombea nafasi ndani ya chama kwa kipindi fulani hadi adhabu zao zitakapo kwisha. Waliopewa onyo kali ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Emmanuel Nchimbi na akitakiwa kuomba radhi huku Mjumbe mwingine Adam Kimbisa akisamehewa.
Wengine waliotimuliwa ni wenyeviti wa CCM Wilaya na wilaya zao kwenye mabano ni pamoja na Omari Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati), Mkolo Laizer (Longido), Abeid Kiponza (Iringa Mjini), Salum Madenge (Kinondoni), Wilfred Soilel Molel (Arusha Mjini), huku Assa Haroun (Ilala) na Hamis Nguli (Singida Mjini) wakivuliwa uongozi wao.
Angalia katika orodha hii jina na wanachama mbalimbali waliofukuzwa na kuonywa na kikao hocho kilichofanyika Dodoma;-