Timu za Sudan Kusini, Burundi zawasili kugombea Kagame

Kagame Cup 201 Tanzania Dar es Salaam

EL Salam Wau ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi zinatarajiwa kuwa timu za kwanza kuwasili nchini kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Michuano hiyo inaanza kutimua vumbi Jumamosi ya Julai 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikishirikisha timu kumi na moja akiwemo bingwa mtetezi Yanga na makamu bingwa Simba.

Kikosi cha El Salam Wau ambacho kitawasili alfajiri ya Julai 11 mwaka huu kwa ndege ya Ethiopia Airlines kikitokea Juba kupitia Addis Ababa, Ethiopia kikiwa na wachezaji 18 na viongozi saba.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Khamis Leone Uso Wani (nahodha), Adheil Bugwic Jongkor Bugwic, Edward Joram Simon Julio, Fidel Andrea Fides Fas, Ismael Musa Juma Ismael, James Anei Matheli Anei, Jervas Ayo Abdalla Ayak, Khamis Doshama Ulama Andel na Meki Sultan Berema Kuku.

Wengine ni Moga Emmanuel Androga, Mubarak Mohammed Saleh Omer, Ndili Rabeh Nasir Hozi, Nizir Rihan Taban Talib, Oliver Paul Kangi Akok, Rabie Mohammed Abubakar Hassan, Rufino Joseph Uras Ambros, Santino Makuei Uyu Upio, Thomas Rufino Thomas Diakon.

Nayo Atletico inatarajiwa kuwasili Julai 11 mwaka huu kwa usafiri wa barabara. Timu hiyo inakuja kwa usafiri wa basi lake ambalo pia italitumia kwa muda wote itakapokuwa kwenye mashindano. Wakati El Salam Wau itafikia kwenye hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo, Atletico itakuwa Lunch Time Hotel iliyoko Mabibo.

Timu zinazotarajiwa kuwasili keshokutwa Julai 12 mwaka huu ni Mafunzo ya Zanzibar kwa boti saa 9 alasiri, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) itatua saa 1.20 usiku kwa Kenya Airways. Timu nyingine itakayowasili siku hiyo jioni ni URA ya Uganda.

Baada ya kinyang’any’iro cha uchaguzi wa Mkutano Mkuu Kata ya Kivukoni wilayani Temeke jijini Dar es Salaam uliofanyika katika viwanja vya Karimjee, pichani ndio walioibuka mabingwa na kuchaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya. Kushoto ni Ndugu Adriano Richard Haonga na kulia ni Ndugu Zulfikar Ali Mzige.
Wakati huo huo; KOZI ya makocha wa mpango wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 imeanza leo (Julai 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.

Wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo wanaoendesha kozi hiyo iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.
Kozi hiyo itakayomalizika Julai 15 mwaka huu inashirikisha washiriki 35, na mwendelezo wa ile ya awali iliyofanyika Desemba 14-17 mwaka jana jijini Dar es Salaam.

Gouinden Thandoo kutoka Mauritius ni mmoja wa wakufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wanaoendesha kozi hiyo.