Timu ya vijana Mara kudumisha nidhamu Copa cocacola


Na mwandishi wetu
Musoma,

TIMU ya soka ya Vijana walio na umri chini ya miaka 17 ya Mkoa wa Mara imeondoka leo alfajiri kuelekea Jijini Dar es salaam tayari kwa kushiriki mashindano ya copa coca cola 2012 huku wakitakiwa kuzingatia suala la nidhamu katika kipindi chote cha mashindano na kuutangaza vyema mkoa wa Mara kupitia mashindano hayo.

Akiiaga timu hiyo hapo jana jioni katika uwanja wa Posta,Katibu wa kamati ya michezo ya Mkoa wa Mara Reuben Luhende alisema hakuna kikubwa kitakachoipa mafanikio ya kufanya vizuri timu bila kuzingatia suala la nidhamu kuanzia kwa makocha,vingozi na wanapokuwa uwanjani wakati wa mchezo.

Alisema kuwa anaamini kwa muda waliokaa kambini makocha watakuwa wamefanya kazi yao kwa umakini mkubwa hivyo kilichobaki ni wachezaji hao ambao watatazamwa na kufatiliwa na wakazi wote wa Mkoa wa Mara kwenda kuwatendea haki na kufanya vizuri na hatimaye kuchukua ubingwa wa mashindano hayo.

Nahodha wa timu hiyo ya Vijana wa Mkoa wa Mara Hassan Ally alisema kutokana na mafunzo waliyoyapata kutoka kwa makocha wanaamini watakwenda kufanya vizuri na kuomba ushirikiano kutoka kwa Wananchi wote wa Mara katika kipindi chote cha mashindano hayo.

Jumla ya wachezaji 20 pamoja na viongozi wanne wameondoka na timu hiyo na mchezo wao wa kwanza umepangwa kupigwa june 24 huku kocha wa timu hiyo James James akiahidi kurudi na kombe la copa coca cola 2012.

Wachezaji walioondoka na timu hiyo ni Mahmoud Zacharia,Daud John,Taro Donald ktoka Town stars,Mosses Shaban,Hassan Itira na Furaha Marcus kutoka Kamnyonge,Allan Aloyce,Edison Julius,Mkama Masatu na HassanAshirafu wa Mwembeni,

Wengine ni Haji Ramadhani na Mfungo Nyamwenda wa Mara Academy,Robert Mapigano wa New Life,Jastine Stanslaus wa Musoma Shooting,George William wa Baruti kids,Baraka Mabeyo wa Bunda kids,Boniphace Damiani wa mafundi kids ya Tarime,Yusuph Sarehe wa amani kids ya Bunda na Israel Daud wa mafundi kids ya Tarime.

Viongozi walioondoka na timu hiyo ni kocha James James,timu meneja Sindbady Madenge,daktari wa timu Nicolaus pamoja na kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mara (FAM) ambaye ni makamo mwenyekiti wa chama hicho na mkuu wa msafara Deogratius Rwechungura.