Timu ya Taifa ya Riadha Wapigwa Tafu na Tanapa

riadha

wanaridha wa Timu ya Taifa ya Tanzania wanaoenda kuliwakilisha Taifa kwenye michuano ya Olimpiki mwaka huu Nchini Brazil wameanza kupata neema baada ya Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) kuwaghalimia malipo ya Bima ya afya kwa mwaka mmoja kabla na baada ya kuondoka Nchini

Mkurugenzi Mkuu wa tanapa Allan Kijazi alisema kuwa wameamua kutoa kiasi cha shilingi Milion tano, Kofia na traki shuti ikiwa ni moja ya kuonesha ushirikiano katika kuhakikisha wanasaidia michezo pamoja na kutangaza utalii nje ya Tanzania wakiamini kuwa kufanya vizuri kwa wanariadha hao ndio moja ya njia ulimwengu kujua hifadha za Tanzania

“Wanariadha hawa ni mfano wa kuigwa katika nchi yetu kwa hivi sasa na Tanapa tutawasaidia ili kuhakiksha wanafanya vizuri zaidi kama ilivyokuwa enzi za kina Bayi, Nyambui na Shahanga ambao hadi sasa Ulimwengu unatambua mchango wao kwenye Riadha nasi tunataka vijana hawa wakaache historia mpya kwenye mashindano ya mwaka huu” alisema Kijazi

Aliongeza kuwa kumekuwa na taarifa kwenye vombo vya habari vya nje ya Tanzania wakiandika Mlima Kilimanjaro upo Nchini Kenya jambo ambalo sio jema kwetu lakini kupitia michezo ya Olimpiki mwaka huu kila mtu atafahamu uhalisia wa hifadhi za Tanania

Kwa upande wake Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka aliongeza kuwa imefika wakati watanzani kuwaamini vijana wao licha ya kuwa na idadi ndogo ya wawakilishi lakini ulimwengu unaweza kugeukia Tanzania pale wanaridha hao watakapokwenda kuonesha umahili wao

“kushindwa kupeleka wanariadha wengi kwenye michuano ya olimpiki mwaka huu haimaanishi kuwa hatutafanya vizuri, ila kwa maandalizi waliyopewa hakuna wasiwasi wa kushindwa kufanya vizuri maana hata wanariadha wenyewe wanakili kuwa wamekamilika kwa ajili ya mashindano hayo”

“tuna pata wakati mgu tunapokwenda kushiriki mashindano makybwa na kujikuta tukitangaza makampuni ya nje ili hali Nchini kwetu kuna makampuni ambayo yangeweza kusaidia hilo, mwaka ujao kuna mashindano ya jumuiya ya madola hivyo hivyo imefika wakati Kutangaza vivutio vyetu” alisema Mtaka

Francis John ambaye ni kocha anayewanoa wanariadha hao kwenye kambi iliyopo west Kilimanjaro alisema kuwa haina haja juu ya kushindwa kufanya vizuri kwa miaka ya nyuma bali watapata majibu na maswali mengine watakaporudi kutoka Brazil

Alphonce Felix ambaye ni mmoja ya wanaridha waliofanikiwa kupata nafasi ya kwenda kwenye michuano ya Olimpiki kwa mara kwanza Akitoa shukrani za pekee kwa Tanapa alisema kwa sasa wanauhakika wa kwenda kufanya kitu cha ziada maana wamegundu taifa linawategemea

“sote ni mara yetu ya kwanza kushiriki michuano hiyo lakini tunauzoefu wa kutosha kwenye michuano mkubwa ulimwenguni hivyo hakuna kitu cha ajabu kitakachotufanya tusifanye vizuri” alisema Felix

Kulingana na kalenda ya Olimpiki ya mwaka huu ratiba inaonesha kuwa michuano hiyo itaanza ijumaa ya Agosti 5 na kumalizika jumapili Agosti 21 huku Tanzania kwa upande wa Riadha tukiwakilishwa na wanariadha wanne pekee wote wa mbio ndefu (Marathoni) ambao ni Fabiani Joseph, Alphonce Felix ,Said Makule na Sarah Ramadhan ambaye ni mwaname Pekee