Na Mwandishi Wetu, Los Angeles
TIMU ya Watanzania waishio Kusini mwa California jana Jumamosi walikutana kwa mara nyingine tena, kwa ajili ya mazoezi kabla ya mechi za mataifa mbalimbali kuanza hapo September 3, 2011 na kumalizika tarehe hiyohiyo. Mashindano hayo yatafanyika jijini Los Angeles, California. dev.kisakuzi.com, ilikuwepo uwanjani kushiriki na pia kushuhudia jinsi timu ilivyokuwa inafanya mazoezi ya nguvu katika upande wa pumzi na viungo, ili kujihakikishia ushindi katika mashindano hayo.
Kapteni wa Bongo Starz, ndg. Jovis Temu alisema, “Inaonekana litakuwa shindano zuri, pia lililopangiliwa. Hamna mtu anayelipwa kushiriki katika mashindano haya, sie wote tunajitolea. Kwa hiyo naomba sana kila Mtanzania na wote wanao ipenda nchi hii waje kujumuika na kushangilia. Mshindi wa kwanza atachukua $3000, kombe moja la timu na medali kwa kila mchezaji. Hili sio kombe la Mbuzi au Ng’ombe” alimalizia kusema.
Bongo Starz itakutana tena Jumamosi ya tarehe 27 na tarehe 28 Jumapili, kabla ya michuano kufanyika Septemba 3. Zifuatazo ni picha mbalimbali za mazoezi hayo.
(Picha zote na Mpigapicha maalum, Los Angeles)