Klabu ya Stand Misuna imepoteza ushindi kwa mechi zote ambazo imemchezesha mchezaji Brown Chalamila kwa jina la Costa Bryan Bosco, kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kadhalika kamati hiyo imepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo wachezaji Brown Chalamila akitumia jina la Costa Bryan Bosco na Adolf Anthon akitumia jina la Fred John Lazaro wamecheza katika mashindano ya ligi ya mabingwa wa mkoa RCL kituo cha Morogoro 2015/2016.
Pia, kamati hiyo imeamua kwamba Seif Juma Maulid ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Stand Misuna FC kupelekwa Kamati ya Nidhamu kwa tuhuma za kughushi na kukamilisha zoezi la usajili kwa udanganyifu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Kanuni ya 53, na kanuni ya 48 (3), 48 (4), 9(21), 36 (6) na kanuni ya 39 (1) adhabu kwa klabu katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL, Kituo cha Morogoro.
Kupitia malalamiko na vielelezo mbalimbali Kamati imebaini kwamba Misuna iliwasajili na kuwachezesha wachezaji Brown Chalamila akitumiaji na la Costa Bryan Bosco (3) na Adolf Anthony akitumia jina la Fred John Lazaro (13).
Wachezaji Brown Chalamila leseni namba 921004001 ni mchezaji halali wa klabu ya Kurugenzi FC ya Mafinga-Iringa na ameichezea Kurugenzi FC ligi ya daraja la kwanza FDL msimuwa 2015/2016. Mchezaji Adolf Anthon leseni namba 950725003 ni mchezaji halali wa klabu ya Singida United na ameichezea Singida United ligi daraja la pili SDL msimu wa 2015/2016.
Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili, waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo wachezaji tajwa hapo juu wamecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Singida na Mashindano ya Ligi ya Daraja la Kwanza FDL na Daraja la Pili SDL ya TFF msimu wa 2015/16.
Katika mchezo namba 42B wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Kurugenzi FC na Lipuli FC uliochezwa tarehe 16/01/2016 uwanja wa Wambi Mafinga taarifa za kamisaa na mwamuzi zimeonesha mchezaji Brown Chalamila (3) alicheza mchezo huo, lakini pia tarehe hiyo hiyo katika mechi namba 3 ya Ligi ya mkoa wa Singida kupitia taarifa za kamisaa na mwamuzi inaonesha kwamba mchezaji Costa Bryan Bosco (3) usajili namba 029 amecheza katika kiwanja cha Namfua Singida katika mechi kati ya Stand Misuna FC na Ruvu Sports Club.
Kamati imejiridhisha bila ya shaka yoyote kuwa mchezaji Brown Chalamila alicheza ligi ya mabingwa wa mikoa RCL 2015/16 kituo cha Morogoro, lakini hawakucheza katika mashindano ya ligi ya mkoawa Singida 2015/2016 na hivyo kupoteza uhalali wa usajili wake kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa.