Timu Nne Zaingia Hatua Ya Pili Guinness Football Challenge

Timu Nne Zaingia Hatua Ya Pili Guinness Football Challenge


*TIMU NNE SASA ZAINGIA KWENYE KIPINDI CHA PILI WIKI IJAYO*

TAREHE 20, Machi katika kipindi cha televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV kila Jumatano ikiwa ni Sehemu ya pili kati ya mfululizo vipindi hivyo halisia, Watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad walionyesha namna ambavyo mtu hapaswi kukata tamaa baada ya kushinda kwa kuwatoa wapinzani wao kutoka Kenya na Uganda katika raundi ya kwanza na kutinga nusu fainali, hatimaye kujinyakulia Dola za kimarekani 5,500 katika ukuta wa GUINNESS.

Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad wameonyesha namna gani kama mwanamichezo hapaswi kukata tamaa uwapo uwanjani na wanamatumaini makubwa kuwakilisha nchi katika mashindano ya Pan African ambapo wanaweza kushinda hadi dola za kimarekani 250,000. Washiriki bora watakwenda kukutana ana kwa ana na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Kenya, na Uganda ili atakayeonyesha ujuzi zaidi atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’ na kupata kitika cha fedha kitakachobadilisha maisha yao.

Washiriki wote wana nafasi kuonyesha ujasiriwa kuipigania nchi yao. GUINNESS ilizunguka katika nchi yetu kusaka washiriki wazuri watakaonyesha umahiri wao wakiwa na matumaini lukuki na timu itakayoonyesha ujuzi zaidi itachaguliwa katika hatua nyingine ya kipindi hiki cha msimu wa pili. Katika Episodi ya pili ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano. Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.

Blue team – Tanzania – Magpies:

Simon Chimbo(21), Emmanuel Temu(20), wote kutoka Dar Es Salaam, ni mashabiki wakubwa wa Manchester United. Simon anasoma Teknolojia ya mawasiliano katika chuo cha Utawala wa Fedha IFM na Emanuel ni mcheza soka kutoka timu ya Mt. Camlius.

Red team – Kenya – Hawks:

Wawili hawa wanatoka Mombasa watavaa mashati mekundu kuonyesha upendo wao kwa mpira wa miguu katika sehemu ya pili Nyuma Donald Otieno (36), atakuwa nguzo ya timu, Awadh Mbarak(22), ataangalia masuala fiziki. Donald ni mwalimu wa soka na Awadh ni mwanafunzi.

Green team – Uganda – Flex:

Mfanyabiashara Ibra Kawooya, (30), kutoka Namusuba na mwenzie Alex Muyobo(31) ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mguu, wote ni mashabiki wa Manchester United.

Black team – Kenya – The Blues:

Francis Ngigi (23), kutoka Nairobi na Kepha Kimani (25), kutoka Thika watakaovalia fulana nyeusi watawakilisha Kenya katika sehemu ya 2. Francis ni Mfanyabiashara na ndo anatarajiwa kuwa kichwa cha Timu.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.

Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia ukurasa huu yaani ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako. Usisahau pia kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.