JUMATANO iliyopita kupitia stesheni za ITV na Clouds TV, Waghana Jonathan Naab na Desmond Odaano walifanikiwa kufuzu nusu fainali ya Pan-African Guinness Football Challenge. Inaweza kusemekana kuwa timu hii ilichagua njia rahisi kwa ajili ya kupata ushindi hadi kufikia hatua ya vikwazo ambapo walikutana uso kwa uso na waghana wenzao.
Jonathan na Desmond walifanikiwa kushinda katika vikwazo vyote na kufikia hatua ya ukutawa pesa wa Guinness ambapo walipata dola za kimarekani 3,000 kuongezea kwenye dola 5,500 walizokuwanazo awali. Wakiwa na jumla ya dola 8,500 mkononi, Jonathan na Desmond wanajiandaa kutafuta dola 250,000 na ushindi wa Pan-African katika nusu fainali ya Guinness Football Challenge.
Watachezea nchi yao pamoja na Emphatus Nyambura na Samuel Papa kutoka Kenya ambao walikuwa washindi wa pili katika robo fainali hyo wiki iliyopita. Katika robo fainali ya mwisho wiki ijayo timu nyingine nne zitaingia uwanjani kati ya hizo ni timu kutoka Kenya Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ambao watapeperusha bendera ya Afrika Mashariki ili kupata timu mbili za mwisho.
“Tumebakiwa na robo fainali moja tu ya Guinness Football Challenge
-Je, kuna moja kati ya timu zilizobaki inayoweza kujishindia dau kubwa zaidi ya timu ya Jonathan na Desmond? Washiriki wote wameonesha kuwa wana ujasiri tutaona jinsi timu hizi nne zitakavyocheza wiki ijayo. Ni nani atakayeshinda katika robo fainali ijayo? Tunazitakia timu zote kila la heri katika robo fainali mwisho” alisema Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi.
Timu zitakazoonesha ujuzi wao katika robo fainali ya mwisho:
• Timu kutoka Kenya Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi katika jezi nyekundu wanaotarajia kushinda baada ya kujitahidi na kupata dola za kimarekani 1,500 hapo awali. Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Cris ambaye ni mchezaji wa Springland FC atakuwa akichezea mpira.
• Maarufu nchini Cameroon kwa kufuata nyayo za shujaa wa kifaransa mwenye majina kama yao Thiery Henry, wachezaji Thiery Teke, kichwa cha timu na Henri Eboule, ambaye ataonesha uwezo wa kucheza soka, wanatarajia kuongeza fedha kwenye zaidi ya dola 5,500 walizokuanazo awali.
• Timu ya pili kutoka Cameroon watakaovaa jezi za kijani ni Botafogo Paul Mbuh na mwanafunzi Remy Isong.Timu hii haikufanya vizuri katika sehemu za awali ambapo walijishindia dola 500 tu lakini sasa ina nafasi ya kufanya vizuri zaidi.
• Katika jezi nyeusi watakuwa Emanuel Kofi Okarku(27) na Isaac Aryee(25) kutoka Ghana. Emanuel na Isaac ni maarufu kwa kushabikia timu mbili adui lakini wanacheza kwa umoja katika timu baada ya kushinda dola 3,000 katika mashindano ya kitaifa. Emanuel ni kichwa cha timu na Isaac atakuwa akionesha utaalamu wa kusakata kabumbu.
Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge barani Afrika wanaweza kupima maarifa yao katika kabumbu kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi. Hakikisha unafuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Robo fainali ya mwisho ya Pan-African itarushwa katika televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.