*Soko la kwanza kwa njia ya mtandao limefunguliwa – Huessein Idd, muhitimu wa fani ya Teknolojia ya Mawasiliano, anauza vifaa vya umeme kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Kaymu.
ANAITWA Hussein Idd, muhitimu wa fani ya Teknolojia ya Mawasiliano katika chuo cha Learn IT. Mapenzi yake kwa Teknolojia ya Mawasiliano hayakuishia chuoni, bali yaliendelea hadi katika kufungua biashara yake mwaka 2010. Jina la duka lake ni Jay’s Infonet Solutions, ambapo anauza vifaa vya umeme, kama vile kompyuta, simu za mkononi, “hard drives”, “flash disk”, na vingine vingi.
Leo hii Hussein anauza vifaa vyake vya umeme kupitia Kaymu, kampuni ambayo ina uwezo wa kusaidi watu wengine pia kama yeye.
“Niliamua kufanya biashara kwa njia ya mtandao kwa mara ya kwanza kwa kuvutiwa na Kaymu, baada ya kushauriana na rafiki yangu nilihisi kwamba kuna uhitaji wa kuwahudumia watu ambao kwa namna moja au nyingine hawana uwezo wa kufanya manunuzi kwa njia ya kawaida – kwa sababu aidha wametingwa na shughuli mbalimbali au wanafurahia tu kununua kwa njia ya mtandao na bidhaa zikaletwa mpaka nyumbani kwao bila wao kusumbuka kwenda mpaka madukani. Kwa hiyo njia pekee ya kulitimiza hili ilikuwa ni kuanza kuuza kwa njia ya mtandao.
Hussein anaelezea jinsi gani kuuza kwa njia ya mtandao kunaweza kuokoa muda na hela, na jinsi gani kunaweza kuwasaidia wauzaji na wanunuaji katika njia chanya sana, kupitia njia salama na ya uhakika ya malipo.
“Kaymu ilinisaidia kukuza kiwango cha biashara yangu kwa kasi sana, na imenipa fursa ya kufanya hivyo bila kutumia nguvu zaidi au uwekezaji zaidi.” Hussein anaendelea. “Unatakiwa tu ufikirie zaidi kuhusu kitu gani unataka kuuza kupitia Kaymu – hasa vitu vinavyouzika kwa haraka zaidi ambavyo watu wanavitumia katika matumizi yao ya kila siku. Hiyo ni muhimu sana lakini nashawishika kwamba kama una bidhaa nzuri, kuuza kwa njia ya mtandao kunaweza kukaleta mabadiliko makubwa katika biashara yako.
“Anaelezea kwamba kukutana kwake kwa mara ya kwanza na Kaymu ambapo wawakilishi wa kampuni walikuja ofisini kwake na kumuelezea jinsi mfumo wake unavyofanya kazi.” “Nilishangazwa na kushawishika sana walipoanza kuongelea kuhusu Kaymu kwa sababu sikuwahi kufikiria kwamba kampuni ya aina yoyote inaweza ikatoa huduma ya namna hii.” Anaendelea, “Sikusita kujiunga kwa sababu nilielewa kiundani ni faida gani ingeweza kuleta kwenye biashara yangu.
Kadri upatikanaji wa intaneti unavyokuwa kwa kasi na pia kwa bei nafuu, kuuza kwa njia ya mtandao Tanzania umeongezeka kwa kasi pia ndani ya miaka miwili liliyopita.
Imekuwa ni ya manufaa sana tangu nilipojiunga nayo na imenifanikisha sana kwani mauzo yangu yameongezeka na nimetambulika sana kupitia huu mtandao. Ni kitu kizuri nilichojiunga nacho na nategemea kuleta vifaa vingine vya umeme mbeleni. Anaelezea maendeleo ya biashara kwa njia ya mtandao Tanzania akijivunia sana yeye kuwa sehemu ya biashara hii.
“Ninajivunia kuwa moja kati ya wachache nchini ambao wataongoza katika mabadiliko ya kidijitali Tanzania”, kwa kadri uchumi unavyoendelea kukua teknolojia nayo inakua pia, kutegemea tu biashara ya njia ya kawaida ya rejareja kutashuka sana. Anahitimisha kwa kuelezea matazamio ya biashara yake jinsi itakavyokuwa katika miaka 5 ijayo. Anahisi kwamba kwa msaada wa kutumia mfumo wa biashara kupitia Kaymu biashara yake itakuwa kwa kasi sana.
“Naona biashara yangu ikiinuka sana, kampuni hii inakua na ninataka duka langu kuwa moja kati ya maduka bora kabisa katika soko hili la mtandaoni”