Tiketi za mabasi ya mikoani sasa kukatwa kupitia simu za mkononi

Picha za simu zikionesha hatua moja baada ya nyingine hadi mteja anapofanikiwa kununua tiketi

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI mpya ya Kitanzania ijulikanayo kama Mobile Ticketing Limited kwa kushirikiana na Mitandao ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, Airtel, Zantel na makampuni ya mabasi inatarajia kuzindua huduma mpya na rahisi ya kukata tiketi (ticket) za mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kwa kupitia simu ya mkononi. Huduma hii ambayo itajulikana kwa jina la “Ticket popote” ni ya kipekee na ya kwanza kuzinduliwa hapa nchini Tanzania.

Mobile Ticketing Limited inatambua usumbufu waupatao abilia wakati wanakata kusafiri za mabasi ya kwenda mkoani na nchi Jirani. Huduma hii inalenga kuondoa utaribu wa kizamani uliokuwa na usumbufu ambapo abilia alitakiwa kufika kwenye ofisi za basi husika ili kukata ticket, kuzidishiwa nauli na madalali (wapiga debe) hasa wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kuuziwa ticket moja mtu zaidi ya mmoja au kuuziwa ticket ya basi lisilokuwa na safari.

Huduma hii mpya ya kukata ticket kwa njia ya ‘ki-electronic’ itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa huu usumbufu, ambapo abilia ataweza kupata tiketi popote pale alipo, kama atakuwa anapata mtandao wa simu husika.

Kupitia njia hii ya ki”electronic” mteja atapiga *150*04# kupata menu ya kukata/kubuku Ticketi na kisha kulipia kwa njia ya M-PESA au mitandao mingine ya Airtel na Zantal ambapo makubaliano na mambo ya kiufundi yapo katika hatua za mwisho. Mteja atatumiwa SMS baada ya malipo kuthibitishiwa na hapo hapo Mteja atapata number ya Ticket, number ya kiti (Seat number) Namba ya basi atakalosafiri nalo, tarehe, muda wa kuondoka na kituo anachoteremkia.

Abiria anaweza kutumia hii meseji kama ticket kwa ajiri ya kupanda Basi(Bus). Kwa abiria wanaohitaji kupata ticket za karatasi (Phyisical ticket) watatakiwa kufika kwenye ofisi zetu Ubungo stendi ya mabasi au Ofisi za basi husika, pia tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha upatikanaji wa tiketi kupitia mashine za Selcom Paypoint kama wanavolipia bidhaa nyinginezo za DSTV, LUKU DAWASCO.

Mpaka sasa Makampuni ya mabasi yapatayo 10 kama ; Metro, Prince, Muro, Saibaba, Ngorika, ABS, Zuberi, NBS na Spider tayari yamejiunga na huduma hii. Mabasi Haya yanafanya safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Tabora, Mtwara. Singida, Dodoma na nchi za Jirani.

Michakato inaendelea ili kuipanua huduma hii kufikia wateja wa mitandao yote ya Simu, Makampuni yote ya mabasi, Mikoa yote nchini na vyombo vingine vya usafiri kama Treni na meli ndani ya muda mfupi.

Huduma kama hii ilishajaribiwa na kufanikiwa katika nchi nyingine za kiafrika kama Nigeria na Kenya. Kwa kuwa watanzania wengi wanajua kutumia vizuri simu za mkononi, nimatarajio yetu kuwa huduma hii itawanufaisha na itaokoa muda wenu ambao huwa mnapoteza kwa ajili ya kwenda kukata tiketi.

Kampuni inawaomba wadau wote hususani Serikari na vyombo vya Habari kuhamasisha umma kuhusu matumizi ya huduma hii kwani faida zake ni pamoja na kuokoa muda, nguvu, fedha na rasilimali nyingine.