Kampuni ya simu ya Tigo, imetangaza uzinduzi wa huduma mpya ya michezo kidijitali ijulikanayo kama Tigo Games. Tigo Games ni huduma katika wavuti ambayo imesheheni michezo mingi kwa ajili ya wateja wa Tigo wenye Smartphone au tablet zinazotumia mfumo wa Android ambao wataweza kupata huduma hii kwa kupakuaApp ya Tigo Games. Kwa wateja wenye simu za kawaida zilizo na intaneti watapata huduma hii katika tovuti ya Tigo Games.
Michezo zaidi ya 800 inapatikana kupitia huduma hii ikiwemo michezo maarufu ambayo ni pamoja na Buddy Man, Cut the Robe, Zombie Run na Tokyo Drift.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “ Huduma hii mpya ya michezo inaifanya Tigo kuwa ya kwanza katika mitandao ya simu Tanzania kutoa jukwaa la michezo linaloweza kutumiwa na watu wengi ambapo wateja wa Tigo wanaweza kucheza michezo mbalimbali kulingana na chaguo lao kwa gharama wanayoimudu.
Tigo imejikita kuendelea kusimamia maslahi ya wateja wake kwa kutoa bidhaa nyingine kwa ajili ya manufaa ya kuwa na simu za kisasa.” “Tigo sasa ndio inaongoza katika upatikanaji wa huduma ya 4G LTE nchini, na kwa sasa huduma hii inapatikana katika miji mikubwa 12.
“Tunaamini kwamba wateja wetu watafaidika sana kutokana na intaneti yenye kasi zaidi itakayo wawezesha kupakua na kucheza michezo hii,” alisema Gutierrez.
Tigo Games ni huduma ambayo mteja akishajua kulipia mara moja, ataweza kuchagua michezo aipendayo na kuicheza atakavyo wakati wowote. Kuna VIP Club ambayo inampa mteja uamuzi wa kujiunga na kifurushi cha siku, wiki na hata mwezi; pia kinamruhusu mteja kupakua michezo bila kikomo.
Mteja ataweza kucheza michezo kwa muda wowote autakao bila makato yeyote. Malipo ya utumiaji wa data kadri mteja anaendelea kucheza ndio yatakayo hitajika. Uzinduzi wa VIP Games Club utakapofanyika, siku 7 za mwanzo wateja wataweza kufurahia huduma bure.
“Kuanzishwa kwa bidhaa hii kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuwapatia wateja wake bidhaa na huduma zilizo na ubora duniani ambazo zinawawezesha kufurahia kwa ujumla maisha ya kidijitali,” alisema Gutierrez.