Tigo mdhamini mkuu Saba Saba 2011

Baadhi ya mabinti maalumu walioandaliwa kutoa huduma mbalimbali ndani ya Banda la Tigo Sa

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Tigo ni mdhamini mkuu wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ya mwaka huu, yanayotarajia kuanza leo katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kufuatia udhamini huo tigo wametoa kiasi cha shilingi milioni nne ambazo zitagharamia muda wa maongezi, simu 20 aina ya blackberry, simu 20 aina ya nokia na makoti maalum kwa ajili ya watu watakaokuwa wakielekeza sehemu za kuegesha magari.
Mkurugezi wa maonyesho hayo ya biashara Ramadhan Khalfan aliiopogeza kampuni ya tigo kwa udhamini wake na kusemakuwa makampuni mengine hayanabudi kuiga mfano wa tigo na kuongezea kuwa yeye binafsi amefurahishwa na hatua hiyo.
Mbali na udhamini huo tigo ilitangaza ofa mbalimbali kwa bidhaa zake kwa wateja wake wote ambao wataweza kutembelea banda la Tigo wakati wa maonyesho ya biashara ya mwaka huu.
Ofisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema kuwa Tigo wana furahia kuwa wadhamini wakuu wa maonyesho hayo na wameamua kutoa ofa kwa wateja wake kama sehemu ya kufurahia matumizi ya mtandao wa Tigo na kuelezea uzoefu wake.
“kila mmoja anajua umuhimu wa maonyesho ya biashara, kwahiyo tumeamua kutumia nafasi hii kutoa ofa kwa bidhaa zetu kama sehemu yakuwashukuru wateja wetu kwa kuchagua mtandao wa tigo. Tunatoa nafasi kwa wateja wetu kufurahia huduma zetu kwa bei nafuu,” alisema.
Alisema kuwa wakati wa saba saba kutakuwa michezo mbalimbali ya bahati nasibu ambayo itatoa nafasi kwa wateja wa Tigo kujishindia zawadi mbalimbali kama vile kompyuta, muda wa bure wa maongezi, simu za mkononi, fulana na bidhaa nyingine kutoka tigo.
“Tumeamua kuuza bidhaa zetu kwa bei ya kawaida ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengine kujiunga na mtandao wa Tigo. Kwa mfano modemu zetu za intaneti zitakuwa zikiuzwa kwa shilingi 15,000/- tu kwa kila moja,” alisema.
Aliongezea kwa kusema kuwa Tigo wanataka kutumia maonyesho ya biashara ya mwaka huu kutangaza zaidi bidhaa zake kama vile huduma ya Tigo Pesa, Tigo Rusha, ambazo zimekuwa kivutio kikubwa cha wateja wake tangu kuzinduliwa kwake.
“Tunazipa kipaumbele bidhaa hizi kwasababu zimekuwa kivutio kikubwa kwa wateja wetu tokea zilipoanzishwa kwahiyo ndiyo maana tunazipa kipaumbele,” alisema Mmbando.
Aidha aliongezea kwa kusema kuwa mwaka huu banda la Tigo litakuwa na mwonekano tofauti na miaka iliyopita “banda letu kwa mwaka huu linamwonekano wa kisasa zaidi ukilinganisha namiaka iliyopita nina imani kwa wale watakaofika hapa watahamini haya ninayosemaleo,” alisema.
“Mwaka huu tuna mnara wa kisasa ambao utarahisisha mawasiliano ya mtandao wa intaneti na pia kuhakikisha kuwa hakutakuwa na kukatika kwa mawasiliano ya simu za mkononi kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo,”
Ends.
Tigo is the first mobile network in Tanzania, which started its operations in 1994. It is part of Millicom International Cellular S.A (MIC) which provides affordable, widely accessible and readily available mobile telephony services to more than 30 million customers in 13 emerging markets in Africa and Latin America. Read more at www.tigo.co.tz